Azam Media wametumia Akili Kubwa sana kuanza na Yanga SC wakati Mkataba watakaouingia na Simba SC utakuwa ni Mnono zaidi

Unajua tatizo la Simba wanamwamini sana yule Zeluzelu,last week Zeluzelu aliwaaminisha kuwa wataipiga Yanga jamaa wakawa full hope kumwamini wakawa wanabetisha hadi wake zao huku mtaani,niwe mwungwana nilimgonga hadi demu wa rafiki yangu maana niliona hawa watu nikuwakomesha tu ! nalogg off wakuu
 
Binafsi mkataba wa Azam na Simba nautazama ktk maeneo mawili

Eneo la kwanza ni endapo mkataba utafungwa kabla ya Simba kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya kuwa Kampuni (kama ilivyotokea kwa Yanga).Hapa ndo kwenye ugumu kwa sababu endapo mkataba utaingiwa kabla ya kukamilika mchakato wa mabadiliko means unakuja kuongeza thamani ya timu,kwa maana hiyo wawekezaji watakaoichukua Simba itawalazimu kufanya uwekezaji angalau utakaozidi thamani ya mkataba pamoja na mali zingine za Club.Kwa mfano sitegemei Simba iwe na mkataba labda tuseme wa 45bil.kwa kipindi cha miaka 10,halafu ikubali uwekezaji wa 25b.Eneo hili Wanunuzi au Wawekezaji hawatalipenda na kwa wale wenye ushawishi wanaweza kufanya "robbing" ili mkataba wa aina usifanyike katika hatua hii kwani gharama za uwekezaji kwa upande wo zinaweza kuongezeka kuliko matarajio ya awali

Eneo la pili ni endapo Mkataba utafungwa baada ya kukamilika kwa mchakato wa Kampuni (tofauti na ilivyofanya Yanga),hapa sasa ndo wawekezaji kama kina MO wanapopataka kwa sababu hapa watanufaika zaidi ,yaani unafanya uwekezaji wa 25b.halafu baada ya Mwezi anakuja mtu mnakubaliana umuuzie sehemu ya uwekezaji wako kwa 45b.tena kwa miaka 10 tu,biashara tamu kabisa hii

Kwa Yanga kuingia mkataba kama huu unapunguza utegemezi wa Wafadhili kwa sababu mchakato wa kampuni bado haujakamilika na huwezi jua nini kitatokea huko mbeleni,,kwa maana ya kwamba leo hii ikitokea labda GSM akaondoka Yanga kabla ya mchakato wa Kampuni haujakamilka timu inaweza angalau kuwa na pa kushikilia isidondoke kama ilivyowahi kutokea miaka miwili iliyopita enzi za kutembeza bakuli

Lakini pia mkataba huu unakuja kuongeza thamani ya Club ya Yanga kabla haijangia kwenye mikono ya Wawekezaji.Yaani mpaka sasa ili wawekezaji waichukue Yanga watahitaji kuwekeza zaidi ya 42b.

Na kwa upande wa Simba kuchelewa kupata mkataba kama huu kunailazimu timu indelee kutegemea Wafadhili kwa sehemu kubwa,na endapo mchakato wa Kampuni hautafika mwisho,na ikatokea MO akakaa pembeni inawezekana timu ikatetereka zaidi kuliko wenzao ambao wana uhakika wa kupata 200m.kila mwezi

............................................
 
ujanja wooote huo,20b kimyaa,uwanja unaitwa sijui nn vile
 
Wewe umetoa kauli kuwa Simba ina products nyingi kuliko Yanga. Hoja sio brands bali ni products zinazozalishwa na Simba naomba nitajie hizo products maana wewe mwenyewe umesema kuhusu products
Timu zake ile ya wanawake na wanaume zote ni mtaji kwa Azam Tv sambamba na ma product mengine mengi under Simba Sc as a Brand
 
Tulivyo kupakueni bao Moja ulipotea kabisa, leo ndio unatokeza na mishedo yako mdomoni.
 
Timu zake ile ya wanawake na wanaume zote ni mtaji kwa Azam Tv sambamba na ma product mengine mengi under Simba Sc as a Brand
Hizo products under simber sc ndio zipi si uzitaje tuzijue sio kuishia kusema tu products under.... Sina shaka na timu za vijana, wanawake na senior team. Bali nataka kujua bidhaa zinazotengenezwa na Simba ni zipi hizo?
 
Kwani thamani ya simba ni kiasi gani tuanzie hapo.
 
Sasa hapo ndipo ujinga wenu ulipo mtajiaminisha kuwa simba inathamini kubwa then mtakataa deal la azam kwakuwa ni dogo then mnalikosa au mnakuwa chini hapo.

Ikiwa Evaluation ya Tapeli Mo itatumika kupata thamani ya simba, basi jiandaeni kisaikologia, Mo alishusha thamani ya simba ili awin kuimiliki simba.
 
Shida yako wewe ni wivu tu,, yaan ukiliona jema la Yanga huwezi kukaa kimya hadi utie husda.
Me sioni cha ajabu hata Simba akila mkataba wa trioni 5 kozi ndo maisha hayo hatufanani hata mishahara ya wafanyakazi inatofautiana hali ya kuwa wote wanafanya kazi ofisi moja.. Yanga inaridhika na inachopata sio kama nyie Mikia.
 
Hawa azam midia huu mkwanja wanaupata wapi? Tff atalipwa 225.6bn, Yanga 43bn , simba 90bn. Jumla 360bn.
Kama unavyodhani Wewe ni Masikini mpaka katika Kope zako za Macho basi kila Mtu yuko hivyo Mkuu? Kuna Watu wana Hela Tanzania hii hii hadi hawajui wazifanyie nini na pia Masikini ( Wanyonge ) tuliotukuka kama akina GENTAMYCINE nasi pia tupo tele tu.
 
Mkuu sikujui 'Personally' ila kwa haya 'Madini' yako ya maana na yaliyoenda Kidato ( Shule ) kwa Heshima yako naomba nikuamkie Shikamoo. Una Akili Kubwa mno na hakika Wewe ni 'Great Thinker' hasa. Kongole ( Pongezi ) nyingi Kwako na nimekukubali sana.
 
Hizo products under simber sc ndio zipi si uzitaje tuzijue sio kuishia kusema tu products under.... Sina shaka na timu za vijana, wanawake na senior team. Bali nataka kujua bidhaa zinazotengenezwa na Simba ni zipi hizo?
Naona tuna mtazamo tofauti stay on your lane
 
Walete Pesa nzuri sio watufananishe na timu ambayo hata CAF CL group stage level hawaijui
 
Hizo products under simber sc ndio zipi si uzitaje tuzijue sio kuishia kusema tu products under.... Sina shaka na timu za vijana, wanawake na senior team. Bali nataka kujua bidhaa zinazotengenezwa na Simba ni zipi hizo?
Mkuu unanifanya nicheke sana kwani umemdaka mwana Simba SC Mwenzangu patamu sana na umeshajua umemkamata na hana cha Kujitetea na Wewe unang'ang'aia hapo hapo tu. Mpambano wenu naufurahia mno huku
 
Unaish kwa imani sana.
Co kila timu itakayoingia mkataba na yanga ni lazima pia kuingia mkataba simba.
Fikiri kwa kutumia akili.Mbona umepatwa na mhaho?
 
Hapo hakuna hoja yoyote,na usidhani kuwa yanga hawajui kuwa,moja ya udhaifu mkubwa wa simba ni uongozi,azqm wanatia saini na nani simba?,mo?au viongozi wa simba?,leo unaiona yanga iko chini,subiri kama mwaka utaiongelea yanga hii hii,unavyoingelea sasa,pia fahamu kuwa azam haina uwezo wa kifedha,kutoa kiasi kikubwa cha fedha hicho kwa timu kubwa 2 nchini tanzania

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Kwa kuchikuchi hotae si alishasema mkia thamani yao ni 4 bilionišŸ˜Ž
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…