Azam Media wekeza pia kwenye eneo la waamuzi wa ligi

Azam Media wekeza pia kwenye eneo la waamuzi wa ligi

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Itakuwa kazi bure kuwekeza sana kwenye timu za ligi luu bila kuangalia pia eneo la waamuzi ubora wa ligi.

Maamuzi mabaya viwanjani yanatia karaha watizamaji wa mpira. Kuna watu wasiopenda karaha wanaoamua wasiangalie kabisa mechi za ligi kuu zenye makosa makubwa ya wazi na makusudi ya waamuzi.

Maamuzi mabaya viwanjani mbali ya kukera watu, lakini pia yanatoa washindi wasioweza kushindana na washindi kutoka ligi nyingine za Africa. Hivyo, eneo la uwamuzi ni muhimu sana kwa Azam Media kwa kushirikiana na wadau wengine kulitupia macho, hasa kwenye mafunzo ya waamuzi na maslahi yao.

Sio vibaya kama Azam Media na TFF utaleta waamuzi kutoka nje kwenye big mechi ili kutoa changamoto kwa waamuzi wetu wa ndani.

TFF na Azam Media mruhusu kutumia Azam tv replays zenu ili kusaidia mwamuzi kuamua makosa yenye utata viwanjani wakati huu ambao hatuna VAR kwenye mechi.
 
Waamuzi watarejesha vipi mzigo watakaopewa na Azam?,iyo inawahusu TFF kwenye mgao waliopewa na Azam wamege fungu huko kwaajili ya waamuzi.
Azam hakusudii kurusha karaha kwa wadau wake. TFF ni sehemu ya sababu ya karaha hiyo pale inapowanga waamuzi wenye madai ya kutolipwa fedha Yao.

Azam na TFF lazima watenge fedha kwaajili ya mafunzo ya waamuzi ndani na nje ya nchi ili kufanya ligi iwe Bora Africa. Branding inahitaji viongizi wanaoangalia nje ya box na sio mahaba ya Simba na Yanga TU.
 
Nadhani wangeweka tv moja uwanjani kwa ajili ya kumuwezesha refarii kupata marudio endapo tukio linautata. Na pia Azam waongeze camera ili kuwesha kuonesha matukio kwa ufasaha kila angle
 
Hoja yako haina mashiko. Azam siyo mdhamini wa ligi na wala msimamizi wa ligi. Sitashangaa ukija na kusema Azam media wawekeze kwenye usajili wa wachezaji wa kigeni kwa timu zote za ligi.
 
Azam hakusudii kurusha karaha kwa wadau wake. TFF ni sehemu ya sababu ya karaha hiyo pale inapowanga waamuzi wenye madai ya kutolipwa fedha Yao.

Azam na TFF lazima watenge fedha kwaajili ya mafunzo ya waamuzi ndani na nje ya nchi ili kufanya ligi iwe Bora Africa. Branding inahitaji viongizi wanaoangalia nje ya box na sio mahaba ya Simba na Yanga TU.
Izo karaha zitakuwepo tu haziwezi kuisha ndo maana Azam wamemwaga mpunga tena wa maana.waamuzi wapo chini ya TFF Azam keshamalizana na TFF ni wao sasa kuweka mazingira mazuri kwenye ligi ili udhamini ujao uwe mnono zaidi.
 
Hoja yako haina mashiko. Azam siyo mdhamini wa ligi na wala msimamizi wa ligi. Sitashangaa ukija na kusema Azam media wawekeze kwenye usajili wa wachezaji wa kigeni kwa timu zote za ligi.
Hakika.
 
Hoja yako haina mashiko. Azam siyo mdhamini wa ligi na wala msimamizi wa ligi. Sitashangaa ukija na kusema Azam media wawekeze kwenye usajili wa wachezaji wa kigeni kwa timu zote za ligi.
Hayo ni mawazo yako ya kijinga. Azam Media wanafanya biashara ya watazamaji wa mpira wa ligi yetu, amewekeza kwenye mpira ili uchezwe vizuri. hakuna mfanyabiashara makini anaependa wateja wake wakerwe na wahuni kama wewe wanaochafua mpira.
 
Mkuu unalzimisha jambo ambalo haliwezekani ni bora ukazie kwa TFF wafanye ilo jambo la kuweka fungu kwa marefa na sio Azam,Azam na marefa wapi na wapi!.
 
Hayo ni mawazo yako ya kijinga. Azam Media wanafanya biashara ya watazamaji wa mpira wa ligi yetu, amewekeza kwenye mpira ili uchezwe vizuri. hakuna mfanyabiashara makini anaependa wateja wake wakerwe na wahuni kama wewe wanaochafua mpira.
Unazidi kuthibitisha upumbavu wako. Azam huyo huyo ana timu inayoshiriki halafu awekeze kwa marefa yeye huyo? Ukishakunywa mataputapu usiandike kitu humu. Basi na GSM wawekeze kwa waamuzi bora pia na MO afanye hivyo hivyo. STUPID!
 
mchango ni mzuri .......c lazima iwe kwa Azam ili kuavoid makelele itafutwe namna t nzuri ya kulifanya Hilo.
 
Hili linawezekana kwa Azam media kuweka tv moja pembeni ya pitch kwaajili ya refarii kupata muda wa kuangalia tukio kwa mfumo wa replay kama ambavyo sisi watazamaji tunavyoona replay kwenye tv zetu. Ils changamoto kwa Azam kuongeza idadi ya camera ili tukio lionekane kwa angle tofauti tofauti ili mtu apate kujiridhisha
 
Back
Top Bottom