Azam Media yatakiwa kulipa Million 100 Kwa Chief Fred Uisso

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, imeiamuru kampuni ya Azam Media Group Ltd kumlipa kiasi cha shilingi milioni 100 mpishi maarufu nchini Master Chef Fred Uisso maarufu kama ‘Mzee wa Maspatasapta’ baada ya kushinda kesi dhidi yake na wenzake watatu baada ya kampuni hiyo kumtangaza mpishi huyo kupitia channel yake ya Sinema Zetu kipindi kinachorushwa na Azam TV

Matangazo hayo yaliyorushwa kwa zaidi ya wiki mbili katika kipindi cha mwezi Agosti, 2023 yalionesha kuwa mpishi maarufu huyo atahudhuria katika tamasha la 'Wapi muziki na misosi Festival 2023' lililoandaliwa na EX-Nihio Ltd kampuni inayomilikiwa na Paul Mashauri

Mpishi huyo maarufu anayemiliki mgahawa wake wa vyakula vya asili uliopo Kijitonyama, aliifikisha kampuni ya Azam Media Group Ltd Ex-Nihio pamoja na Paul Mashauri katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kwa madai kwamba wadaiwa hao wameupotosha umma kwa kuwahadaa kuwa atashiriki katika tamasha hilo suala ambalo si la kweli

Katika Mahakama ya Kisutu Master Chef Fred Uisso aliiomba Mahakama kuwataka wadaiwa kumlipa fidia ya madhara ya jumla kwa kuwa matangazo yake yaliuhadaa umma suala lililopelekea kukosa biashara katika mgahawa wake

Hivyo, Mahakama baada ya kusikiliza shauri hilo kwa takribani mwaka mmoja Agosti 16.2024 imefikia maamuzi kwa kuwataka washtakiwa kumlipa fidia ya madhara ya jumla kiasi cha shilingi milioni mia moja (100,000,000/-) pamoja na gharama za uendeshaji wa shauri hilo.

Akizungumza Wakili Ferdinand Makore aliyemuwakilisha mdai, mara baada ya kutoka Mahakamani hapo, amesema:

“Haya maamuzi ya leo yanatoa fundisho kwa watu wote wanaopenda kutumia majina ya watu kwa ajili ya umaarufu wa majina hayo, kwa kuwaaminisha umma kuwa fulani atakuwepo, suala ambalo mara nyingi huwa ni uongo na hufanya hivyo kwa lengo la kupata watu wengi” -Wakili Makore

Chanzo.Wanasheria
 
Ukisomea Sheria, Raha sana magap ya hela hayakupiti
Inaonekana kwamba suala hili kama lilikuwa dili la kutengenezwa ili kumkomba pesa Mzee Bakhresa.
 
Kacheza kama Mwana FA na AY waliovuna mabilioni toka kampuni ya simu iliyotumia wimbo wao (mbayaaa) bila idhini yao
 
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, imeiamuru kampuni ya Azam Media Group Ltd kumlipa kiasi cha shilingi milioni 100 mpishi maarufu nchini Master Chef Fred Uisso maarufu kama ‘Mzee wa Maspatasapta’ baada ya kushinda kesi dhidi yake na wenzake watatu baada ya kampuni hiyo kumtangaza mpishi huyo kupitia channel yake ya Sinema Zetu kipindi kinachorushwa na Azam TV

Matangazo hayo yaliyorushwa kwa zaidi ya wiki mbili katika kipindi cha mwezi Agosti, 2023 yalionesha kuwa mpishi maarufu huyo atahudhuria katika tamasha la 'Wapi muziki na misosi Festival 2023' lililoandaliwa na EX-Nihio Ltd kampuni inayomilikiwa na Paul Mashauri

Mpishi huyo maarufu anayemiliki mgahawa wake wa vyakula vya asili uliopo Kijitonyama, aliifikisha kampuni ya Azam Media Group Ltd Ex-Nihio pamoja na Paul Mashauri katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kwa madai kwamba wadaiwa hao wameupotosha umma kwa kuwahadaa kuwa atashiriki katika tamasha hilo suala ambalo si la kweli

Katika Mahakama ya Kisutu Master Chef Fred Uisso aliiomba Mahakama kuwataka wadaiwa kumlipa fidia ya madhara ya jumla kwa kuwa matangazo yake yaliuhadaa umma suala lililopelekea kukosa biashara katika mgahawa wake

Hivyo, Mahakama baada ya kusikiliza shauri hilo kwa takribani mwaka mmoja Agosti 16.2024 imefikia maamuzi kwa kuwataka washtakiwa kumlipa fidia ya madhara ya jumla kiasi cha shilingi milioni mia moja (100,000,000/-) pamoja na gharama za uendeshaji wa shauri hilo.

Akizungumza Wakili Ferdinand Makore aliyemuwakilisha mdai, mara baada ya kutoka Mahakamani hapo, amesema:

“Haya maamuzi ya leo yanatoa fundisho kwa watu wote wanaopenda kutumia majina ya watu kwa ajili ya umaarufu wa majina hayo, kwa kuwaaminisha umma kuwa fulani atakuwepo, suala ambalo mara nyingi huwa ni uongo na hufanya hivyo kwa lengo la kupata watu wengi” -Wakili Makore

Chanzo.Wanasheria
Rekebisha: Ni Chef na sio chief
 
Hivi huyo Mzee si alikuwa anahost kipindi Cha Masaptasapta Azam.. kwahyo kawazingua waajiri wake..?
 
Back
Top Bottom