Azam media

astranaut

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2018
Posts
1,276
Reaction score
1,024
Kuiga kitu kizuri kwa mwenzio sio vibaya ndio maana Leo China yuko vile kwa sababu alikubali kuiga na kucopy teknolojia kwenye maonesho ya kwanza ya sayansi na teknolojia yaliyofanyika nchini uingireza mwaka flani karne ya upinduzi wa viwanda.

Hivyo basi azamtv kwakua nyie mmeingia kandarasi ya kuonesha burudani nchini hasa upande wa michezo sio vibaya mkawa mnaiga vitu vingine super sport namna ya kuboresha vipindi vyenu hasa hizi channel zenu zinazoonesha Mpira,vitasa n.k

Mfano supersport wana channel yao inayo itwa supersport bllitz,hiyo ni mahususi kwa kurusha habari zote na udaku wa ligi mbali mbali.Hapa ndipo hasa kipindi hiki cha usajili utapata habari zote na udaku wote wa magazetini kuhusu sajili zinazofanyika kwenye ligi duniani na mashindano mengine.

Hivyo basi na nyie fanyeni namna kama ni kuongeza channel nyingine au miongoni mwa zilizopo hasa kipindi hiki cha dirisha LA usajili mkawa na channel mahsusi kwa ajili ya kazi hiyo.
Taarifa za ligi kuu,kikapu,vitasa,mashindano ya magari,n.k ukanda wote wa afrika mashariki tuwe tunazipata huko.
 
Gharama kuanzisha chaneli mpya, lakini pia fursa ya ajira kwa vijana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…