Pesanyingi
JF-Expert Member
- Apr 15, 2023
- 1,157
- 1,983
Kwa nafasi ya uwakilishi wa kuwa na timu nne bado tumeshindwa kuwa na timu zenye ushindani. Timu zinazopata nafasi ya kuwakilisha nchi kwa michezo ya kimataifa hazijajianda au hazina utayari zaidi ya BAHATI na si ubora.
Tumeshudia Azam na Coastal Union walichofanya hatua za awali tu wameshindwa vibaya kusonga mbele na hili si mara ya kwanza kila tunapopata nafasi ya kushirikisha timu nne hali ni tete.
Ni bora kuwa na timu moja au mbili zinazoonesha kupambana kuliko kuwa na timu nyingi ambazo hazijui zinataka nini.
Tusijisifu kuwa ligi yetu ni bora kwa sasa kuna sehemu tunapobahatisha siyo kwa uwezo, au soka la Afrika tuseme limeshuka viwango nasi tunapita kwenye mwanya huo huo.
Katika wanne, wawili ambao ni dhaifu na wameonyesha udhaifu wao tayari washarudi kuendeleza porojo zao, wa tatu nae yupo kwenye hati hati muda wowote kwani bado anajitafuta. Na wa mwisho na imani hatotudhalilisha kazi yao inaonekana wazi wazi bila chenga.