Azam rekebisheni hii(la liga)

maiyanga1

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
1,340
Reaction score
1,832
Habari wakuu, naangalia mechi kati ya Real Madrid na Eibar mpira unatangazwa kiswahili. Unaweza kuchagua lugha kati ya kiswahili na kiingereza, lakini kotekote wanatangaza kiswahili, tatizo nini? Hii pia hutokea katika baadhi ya mechi za Uingereza wanazoonyesha.
Kuna raha yake kusikia wanavyotangaza wenyewe kwa lugha ya malkia hata kama mengine yanatupita kuliko kusikiliza vitu na majina tofauti ya wachezaji.
 
Dah binafsi baadaya ya lile goli la kroos nikaenda kulala maana hata mzuka ulikata huyo ulamaa hakuona wala kujua ni goli aligundua baada ya kuona wanashangilia naye ndo akaanza kushangaa
 
Nikweli mkuu,hata mzuka unakosekana maana mtangazaji anakuwa tabata anaangalia kama mm nyumbani,akishaona tukio ndiyo anatangaza,haina haja
 
Mkuu hii kitu huwa inanipa taabu sana,wakati mwingine hata mpira hawatangazi, wanaishia kusifia mchezaji mmoja.AZAM wamenipelekea ninapoangalia La Liga niondoe sauti,bora niangalie mpira huku nasikiliza redio kuliko ule ujinga wa Watangazaji wao.
 
Haifai kabisa kusitisha matangazo ya moja moja kutoka uwanjani. Sijui nani aliwadanganya kuwa watazamaji tunafurahia kutangaza kwa kiswahili
 
Naam tunashukuru kwa kero mnazozipata tutazifanyia kazi, endelea kufuatilia azam tv.
Kiswahili tuliwawekea watu wa Geita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…