Azam, Simba & Yanga

Azam, Simba & Yanga

madeinmusoma

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
324
Reaction score
387
Nina uwezo mkubwa wa kucheza kandanda, na nikisimama namba 10 namba 9 atatupia tu atakavyo. Natamani kucheza hizo vilabu vya ligi kuu bara.

USHAURI TAFADHARI!
 
Anzia kwenye timu ndogo ndogo au nenda zanzibar then hizo timu zitakuona halafu kiongozi mmojawapo wa hizo timu akizungumza na wewe hata kama sio mambo ya usajili wewe tangaza kwenye magazeti timu yake inakutaka kukusajili ghafla utakuwa lulu timu zote zitakugombania na dau la usajili halitapungua millioni 20 na mshahara mzuri.

Au ikitokea mojawapo ya hizo timu ina mechi ya kirafiki na timu utakayochezea wewe jitahidi uwafunge lazima wakusajili kwa sababu wao hawana scouting wanaangalia tu mchezaji aliyewasumbua au aliyesumbua timu pinzani basi. Ukiwa na huu mkakati mwaka mmoja tu tutakuona simba, yanga au azam.
 
Una umri gani??Km bado ni kijana mdogo/kinda nenda simba au azam ktk zile timu ndogo zao then baada ya mwaka 1 au 2 utakuwa hupo tayari kuchezea timu ya YANGA NA TAIFA STARS.Hizo timu zina program nzuri kiasi katika kukuza wachezaji so ukienda hapo mambo yako yatakuwa safi baada ya muda mfupi tu.
 
Kuchezea timu kubwa ulizozitaja hapo juu kunahitaji vitu vingi sana.UMESHACHEZA ANGALAU LIGI DARAJA LA KWANZA??Natumai hizo ndio njia sahihi kwa mfumo wa soka letu yakupasa upite huko na ufanye mazoezi kweli kweli hili ufikie malengo yako.
 
Back
Top Bottom