N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,427
- 10,905
Nikiangalia televisheni za wenzetu za michezo hasa za super sport wenzetu huonyesha Marathon mbalimbali kwenye miji lakini hapa kwetu Azam kupitia chaneli zake imekuwa ikijikita zaidi kwenye soka na kidogo siku za karibuni wamekuwa wakituonyesha masumbwi.
USHAURI WANGU KWENU
Hizi jogging na Marathon zinazofanyika kwenye miji mbalimbali hapa kwetu Tanzania nashauri muwaze kuzirusha live ili kuhamasisha michezo miongoni mwa jamii zetu. Aidha nawaza mnaweza kuwasiliana na waratibu wa matukio haya ili kupata sponsors na hii ikawa fursa mpya ya biashara lakini yenye manufaa kwa jamii yetu.
Aidha wekeni utaratibu wa kutuonyesha live matukio kama mbio za magari zinazofanyika kila mara huko Arusha Kilimanjaro, Mwanza, Iringa na kwingineko. Pia tumekuwa na michezo ya mbio za Baiskeli kule Mwanza tunaomba muyaweke kwenye programu ya kutuonyesha live itafaa sana. Hizi ni fursa zitumieni mtupe raha.
------
Kwani hii dunia ni yetu?