Azam TV boresheni matangazo ya mpira upande wa picha za marejeo

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Sijui shida ni idadi chache ya camera ila kitu gani ambacho kinashindwa kufanya matukio yenye utata yawekwe wazi kupitia picha za marejeo.

Hili watu wameliongelea tokea misimu ya nyuma, tulivyoona kuna ununuzi wa VAR, na camera mpya tulitegemea matukio yenye utata viwanjani vimepata mkombozi kwa angalau ila ni vile vile tu.

Goli la leo lililofungwa na Bacca kwa marejeo ya video inaonesha kuwa hakuna kichwa kilichopigwa, lakini kuna mikono ya watu watatu imeongozana akiwepo kipa wa Prisons, Bacca na mchezaji wa Prisons ila huoni ni yupi mtu wa mwisho kuugusa ule mpira ni mchezaji yupi bali unaona tu papatu papatu halafu mpira ule unaenda nyavuni.

Raha ya kuangalia mpira kwenye TV ni wote kuondoka na jibu la aina moja kupitia marejeo ya video. Sasa haijulikani kipa alijifunga, au mchezaji wa Prisons kaunawa mpira au mchezaji wa Yanga ndiye aliyeunawa mpira. Nimetazama video zaidi ya mara tano hali clarify tukio la goli 4 la Yanga.

View: https://x.com/SportsarenatzTz/status/1870844096933495220?t=f3-Bzz7DNfdmMv2RrguVuA&s=09
 
Goli ni la mkono hilo tu ndio ambalo tunaweza kuthibitisha

Ujinga upo kwa hao wachezaji wa Prisons ambao hakuna hata aliyenyoosha mkono kumpa ishara refa kuwa kuna Maradona wa Jangwani kafanya ufuska.

Yameinamisha vichwa chini kama kalunguyeye, incidents kama hizi hata kama zinatokea kwa bahati mbaya ndio zinawapa nguvu wale watu wanaosema udhamini wa GSM unaharibu ushindani halisi wa mpira.
 
Kwavile umeongelea ishu nyeti ya uthibitisho basi naomba weka hapa screen shot ya mpira wakati ukiwa katika mikono ya Bacca.
 
Angalia hapo kulikuwa na battle ya watu wawili kugombania mpira.

Watu wote wawili walikuwa wametanguliza mikono mbele, mmoja ni kipa huyo niliyemzungushia mstari mwekundu ambaye ndio ana uhalali wa kutumia mikono na mwingine ni Bacca nimemzungushia na mstari wa kijani
Screenshot (1) copy.jpg

Halafu katikati yao kuna mpira ambao nimeuzungushia na mstari mweupe.

Kwa hiyo kipa angeufikia ule mpira basi unge change direction kutoka kuelekea aliposimama line 2 (nimemzungushia duara jeusi) na kufanya uelekee lango la mpinzani ambaye ni Yanga.

Lakini kwakua Bacca ana mikono mirefu kama ya mwizi alikuwa wa kwanza kuucheza ule mpira na ndio maana ulielekea golini kwa Prison
 
View attachment 3182755

Ukiangalia kwenye angle hii utaona mikono yote mitatu ilikuwa pamoja ( wa kipa,Bacca na mchezaji wa Prisons)
Halafu hata kwenye screen shot yako inaonesha kipa ndiye mwenye mikono mirefu na ndiye aliyetangulia kuugusa mpira. Kuubadili mpira direct inatokana na namna ukaaji wa mkono wake ulivyouweka. Hivyo hata kipa anaweza kuhusika katika kuubadilisha mpira mwelekeo kwa lengo la kuudaka
 
Kwamba kipa ndiye aliyeucheza mpira halafu mpira ukarudi nyuma licha ya kwamba direction ya mikono yake iliekea mbele?

Una maelezo mengine ya ziada ambayo naweza nikayasoma tofauti na huu mzaha uliondika?
 
Azam sjui huwa hawaoni kwenye mechi za ulaya
Mechi za Ulaya sio mwenye kituo cha tv anayeonesha hayo matukio bali ni ligi yenyewe ndio inayoajiri.

Inatakiwa kuwe na camera permanent kwenye viwanja kwa ajili ya matukio kama haya, camera za Goal line technology, VAR, offside etc
 
Goli ni la mkono hilo tu ndio ambalo tunaweza kuthibitisha

Ujinga upo kwa hao wachezaji wa Prisons ambao hakuna hata aliyenyoosha mkono kumpa ishara refa kuwa kuna Maradona wa Jangwani kafanya ufuska.

Yameinamisha vichwa chini kama kalunguyeye, incidents kama hizi hata kama zinatokea kwa bahati mbaya ndio zinawapa nguvu wale watu wanaosema udhamini wa GSM unaharibu ushindani halisi wa mpira.
Kwani tumeshayasema timu za majeshi kwa yanga ni mlenda wanapokea maagizo tu!
 
Goli ni la mkono hilo tu ndio ambalo tunaweza kuthibitisha

Ujinga upo kwa hao wachezaji wa Prisons ambao hakuna hata aliyenyoosha mkono kumpa ishara refa kuwa kuna Maradona wa Jangwani kafanya ufuska.

Yameinamisha vichwa chini kama kalunguyeye, incidents kama hizi hata kama zinatokea kwa bahati mbaya ndio zinawapa nguvu wale watu wanaosema udhamini wa GSM unaharibu ushindani halisi wa mpira.
Mi niko tofauti kidogo asee, yani nikianzaga kusikia kelele za GSM najua Yanga imeanza kuimarika.

Though goli ni la mkono. Sisi wa kwenye Tv tumeliona baada ya marudio sio vyema kuwalaumu sana wa uwanjani.
 
Utata mwingi unatokea eneo la golini Cha ajabu hakuna jitihada za kuongeza camera eneo hilo
 
Sina utaalam na mambo ya video broadcasting ila nahisi camera zao zina frame rate ndogo so ni ngumu kunasa matukio vizuri...
 
Ina maana azam walishashindwa kununua camera za slow motion
Inawezekana na inamaanisha bei ya vifurushi na visimbuzi ipande.

THE HIGHER THE QUALITY, THE HIGHER THE PRICE.

Je, hatutawaita wapigaji kama kawaida yetu?
 
Sijui shida ni idadi chache ya camera ila kitu gani ambacho kinashindwa kufanya matukio yenye utata yawekwe wazi kupitia picha za marejeo.

Hili watu wameliongelea tokea misimu ya nyuma, tulivyoona kuna ununuzi wa VAR, na camera mpya tulitegemea matukio yenye utata viwanjani vimepata mkombozi kwa angalau ila ni vile vile tu.

Goli la leo lililofungwa na Bacca kwa marejeo ya video inaonesha kuwa hakuna kichwa kilichopigwa, lakini kuna mikono ya watu watatu imeongozana akiwepo kipa wa Prisons, Bacca na mchezaji wa Prisons ila huoni ni yupi mtu wa mwisho kuugusa ule mpira ni mchezaji yupi bali unaona tu papatu papatu halafu mpira ule unaenda nyavuni.

Raha ya kuangalia mpira kwenye TV ni wote kuondoka na jibu la aina moja kupitia marejeo ya video. Sasa haijulikani kipa alijifunga, au mchezaji wa Prisons kaunawa mpira au mchezaji wa Yanga ndiye aliyeunawa mpira. Nimetazama video zaidi ya mara tano hali clarify tukio la goli 4 la Yanga.

View: https://x.com/SportsarenatzTz/status/1870844096933495220?t=f3-Bzz7DNfdmMv2RrguVuA&s=09

Hao ni media partner na Utopolo
 
Back
Top Bottom