Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mtangazaji wa Azam TV Faraja Kiongole na Mwandishi katika Kipindi
Maalum cha Mashujaa
Video itawekwa hivi karibuni In Shaallah...
Katika kipindi hiki nilijaribu kueleza historia ya baadhi ya mashujaa ambao wanahistoria wamewaacha kuwatafiti na kuwaandika kwa makusudi au kwa kutojua michango yao. Katika maelezo yangu picha za mashujaa hawa ziliwekwa kwenye screen ya TV.
Naziweka baadhi ya picha hizi hapo chini:
Walioasisi TANU tarehe 7 Julai 1954
Kushoto: Iddi Faizi Mafongo Mweka Hazina wa TANU Makao Makuu,
Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo, Mwalimu Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro
mmoja wa waasisi wa TANU 1954, Haruna Taratibu Muasisi wa TANU Dodoma.
Picha hii ilipigwa Dodoma mwaka wa 1956
Picha hii inaeleza historia ya Rashid Ali Meli mzalendo aliyefungua ''safe,'' ya kazini kwake Dar es Salaam Municipal Council alipokuwa akifanyakazi kama mwekafedha akatoa fedha zote na kuzipeleka kwa Iddi Faizi Mafongo zitiwe katika safari ya Mwalimu Nyerere UNO mwaka wa 1955. Rashid Ali Meli alifanya haya baada ya kuona kuwa juu ya michango iliyopita lakini fedha za safari zilikuwa hazijakamilika. Ilikuwa TANU warejeshe hizi fedha kwa haraka. Bahati mbaya sana siku ya pili tu wakaguzi wakafika kumkagua ilhali fedha haijarejeshwa. Huu kwa macho ya sheria ilikuwa ni wizi. Katika kipindi nimeeleza nini kilitokea.
Historia ya Iddi Faizi Mafongo na Haruna Taratibu zinapatikana hapo chini:
Mohamed Said: Idd Faiz Mafongo Mweka Hazina wa Safari ya Nyerere UNO 1955
Baraza la Wazee wa TANU 1955
Hilo hao juu ndilo lilikuwa Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti Sheikh Suleiman Takadir. Baraza hili lilikuwa ni baraza ambalo wajumbe wake wote walikuwa Waislam. Hili ndilo baraza lililompeleka Nyerere UNO mwaka wa 1955. Nyerere aliamua kulivunja hili baraza mwaka wa 1963 kwa kuwashutumu kuwa wazee hawa walikuwa wakichanganya dini na siasa.
Kulia: Ali Msham na aliyekaa katika meza ni Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere siku Ali Msham alipomkaribisha kwenye tawi la TANU Magomeni
alilofungua nyumbani kwake mwaka wa 1955
Ali Msham alikuwa mwenyeji wa Kilwa na alihamia Dar es Salaam katika miaka ya 1950 kuja kutafuta maisha. Alifungua ''workshop,'' yake Kariakoo akitengeneza samani. Harakati za uhuru zilipoanza yeye alifungua tawi la TANU nyumbani kwake Magomeni Mapipa Mtaa wa Jaribu. Siku moja alimtembelea Mwalimu Nyerere ofisini kwake New Street akasikitishwa na ile samani aliyoikuta katika ofisi ya Nyerere. Msham akaamua kumtengenezea Mwalimu Nyerere samani inayokwenda na hadhi ya rais wa TANU. Ilipokamilika alimualika Mwalimu Nyerere kwenye tawi lake la TANU ili amkabidhi zile samani ambazo ndiyo hizo hapo kwenye picha.
Historia ya Ali Mshama iko hapo chini:
Mohamed Said: PICHA ADIMU ZA TANU, JULIUS NYERERE NA WAZALENDO WALIOSAHAULIKA KATIKA HISTORIA YA KUDAI UHURU WA TANGANYIKA 1954 - 1961
Mohamed Said: ALI MSHAM, TAWI LA TANU NA DUKA LA MAFUTA YA TAA LA MAMA MARIA NYERERE
Mohamed Said: KUTOKA FACEBOOK: ALI MSHAM NA JULIUS NYERERE 1955
Mohamed Said: KUTOKA FB: MJADALA WA ALI MSHAM NA JULIUS NYERERE
Earle Seaton na Julius Nyerere
Earle aliisaidia sana TAA wakati uongozi ulipochukuliwa na vijana mwaka 1950 akifanya kazi kwa karibu sana na TAA Political Subcommittee hasa katika mambo ya sheria inayohusu makoloni yaliyokuwa chini ya udhamini kama Tanganyika ilivyokuwa chini ya udhamini wa Uingereza. Seaton alikuwa raia wa Bermuda na mwanasheria akifanya shughuli zake Moshi.
Habari za Earle Seaton hapo chini:
Mohamed Said: KUTOKA JF: EARLE SEATON (BERMUDA) NA DOME BUDOHI (KENYA) KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA
''Prison Graduate'' Robert Makange
Katika pilikapilika za kupambana na ukoloni wa Waingereza wako wazalendo walifungwa jela, Mwaka wa 1953 Ali Migeyo alipigwa mabomu Kamachumu wakati akihutubia mkutano wa hadhara. Alipelekwa mahakamani na akahukumiwa kifungo. Robert Makange na Rashid Kheri Baghdelleh walihukumiwa kifungu cha miezi sita kwa kosa la kuandika makala katika gazeti la Mwafrika makala ambayo Waingereza waliiona ni ya ''uchochezi.'' TANU kwa kuchukia kuona wanachama wake wanaitwa wafungwa waliwapa jina la, ''Prison Graduates,'' yaani, ''Wahitimu wa Jela.''
Soma historia ya Ali Migeyo hao chini:
Mohamed Said: Ali Migeyo: Ushapata Kumsikia Shujaa Huyu Aliyepigania Uhuru wa Tanganyika?