Azam TV kuanza kuonesha Kombe la FA ya Uingereza mwakani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564



KATIKA kuhakikisha Azam TV inakidhi mahitaji na matakwa ya wateja wao, Kampuni ya Azam Media itaanza kurusha matangazo ya mechi za Kombe la FA la England.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza katika hatua ya tatu Januari 4, mwakani ambapo baadhi ya mechi zitakazoonyeshwa ni Man United v Reading, Wolves v Liverpool , Man City v Rotherham, Chelsea v Nottingham Forest na mshindi kati ya Solihull Moors na Blackpool v Arsenal.

Azam itaungana na wapenda soka duniani kote kukuletea michuano hiyo mikongwe iliyoanzishwa mwaka 1871.

Kombe la FA maarufu kama Emirates, huzikutanisha timu za madaraja mbalimbali England.

“Hii ni hatua nyingine muhimu ambayo Azam TV tumechukua kuhakikisha wateja wetu wanafurahia burudani ya soka sebuleni kwao na popote walipo. “Hata kupitia simu zao za kiganjani ‘Smartphone’ kupitia programu tumishi ya Azam TV App inayopatikana bure bila malipo yoyote.

Hakika hii ni zawadi tosha ya mwisho wa mwaka kwenu wateja wetu wa Azam TV,” alisema Mkurugenzi wa Azam TV, Tido Mhando.


You May Like
 
Waweke kwenye kifurushi cha bei nafuu
 
sema azam tv wanalamikiwa kitengo cha suport service call centre.sijui wahudumu wanalalaga ikifika mida flan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…