Azam TV: Mapinduzi ya Zanzibar kutoka kumbukumbu zilizozikwa

Hivi huyu pascal anahadhi ya kuitwa mwandishi kweli! Maana inaonekana huwa anahoja nyepesi na zenye lengo La ubishi na kubuy time tu

Au ndo uandishi wa mtandaoni(kila MTU mwandishi)!?

Embu leta kazi zako zinazotokana na primary source km mzee Mohammed anavyofanya
 
Pasco anazingua yeye source zake anakwambia "nimehadithiwa" hahaaa yan mwandishi zima anatupa source great thinker za kusimuliwa, mwenzako anatupa vitabu. Ameenda mbaaali anatupa link za maandishi yake ya nyuma! Pasco Kuwa criaz bn. Maandiko yako yanawezaje kuwa biography and references tena hata ithibati hayana.
 
Azam TV inaleta revisionist theory za hawa waarabu .Mapinduzi ya Zanzibar ni tukio lililompa mwafrika uhuru baada ya mamia ya miaka ya kutawaliwa na kufanywa mtumwa na fe hdhuri mwarabu.

Sasa inashangaza bado kuna watu leo hii wanatetea Unyama wa waarabu.
 
Kwenye kipindi cha Tuongee asubuhi cha Star TV, siku ya Mapinduzi, alialikwa mzee Mkinga kujadili kama dhima ya Mapinduzi imefikiwa.
Kikubwa alisema kuwa imefikiwa kwa kuwa hakuna tena watwana na kila mtu ana haki mbele ya sheria, achilia mbali maendeleo makubwa yaliyoletwa na serikali zote hizo baada ya Mapinduzi.
Ila mzee Mkinga aliongeza kitu kimoja kuwa yapaswa waandishi wanaopotosha Mapinduzi yale washughulikiwe na maandishi ya vitabu vyao yasiruhusiwe kokote ndani ya JMT.

Alitolea mfano wa kitabu alichokuwa nacho mkononi cha" Kwa heri ukoloni cha mwandishi Ghasani.
Kwa maoni yake hao kina Ghasani na kina Mudi wote waangaliwe vyema maana maandishi yao yana matokeo hasi
 
Kwa humu jf, mimi ni mwandishi tuu wa mtandaoni, na specialization yangu sio uandishi, ila kwa kule kwenye speciality yangu na mimi pia ni nguli kama alivyo Mzee MSA katika uandishi wa vitabu.

Paskali
 
Kwa kiwango cha mkinga hiyo ilikuwa mada kubwa kwake maana hana uweledi NATO sana sana itakuwa alitoka povu tu
 
Nashindwa kufahamu sikuzote. Kwanini wabongo wanakua na hasira na uarabu na kuchukia usultani kuliko hata ao wazanzibari wenyewe. Ikiwa wazanzibari wenyewe hawana tatizo na uarabu wala usultani. Na wala hawana mpango na mapinduzi. Kwanini wabongo wao ndo wanakua wanaumwa na mapinduzi na kua na chuki na hasira dhidi ya uarabu na usultani?
 
Nawatakia kumbukumbu njema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyovikomboa visiwa hivi.
P
 
Nawatakia kumbukumbu njema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyovikomboa visiwa hivi.
P
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
 
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Mwana JF, Paskali, anakutakia wewe na familia yako HERI YA SIKUKUU YA MAPINDUZI MATUKUFU
YA ZANZIBAR!
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…