Azam Tv Morning Trumpet Karume Day 2015 Mahojiano Kati ya Irene Kilenga na Mohamed Said

Azam Tv Morning Trumpet Karume Day 2015 Mahojiano Kati ya Irene Kilenga na Mohamed Said

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
AZAM TV KARUME DAY: ABEID AMANI KARUME - "THE MASTERMIND" MAHOJIANO NA IRENE KILENGA 2015
Picha hiyo hapo chini ya Mzee Abeid Amani Karume ilipigwa Dar es Salaam mwaka 1948.

Kushoto waliokaa ni Hassan Machakaomo, Selemani Mwinyimadi Chambuso, Mohamed ''Mabosti'' Sultan.

Waliokaa kwenye viti kushoto wa kwanza jina halikupatikana, Rajab Swedi, Khamis Shari, Abeid Amani Karume, Kondo Salum Kipwata, Mtaruke Mangara, aliofuatia jina halikupatikana.

Waliosimama Abdallah Mzee, Chonjo Mwinchande Digendo, Juma Ismail, Shaaban Bajuni, anaefuatia jina halikupatikana, Khamis Mjinga, Selemani Mohamed, Mtoro Rehani, Mangara Tabu Mangara, Ali Majaliwa.

Hawa walikuwa viongozi wa Young Africans Football Club, maarufu kwa jina la Yanga.
(Picha hii ni kwa hisani ya Mwinyi Mangara mwana familia ya ukoo maarufu Dar es Salaam wa Mangara).

Asubuhi ya tarehe 17 Aprili, 2015 nilifanya kipindi maalum cha Rais Abeid Amani Karume (1905 - 1972) "The Mastermind," na Irene Kilenga wa AZAM TV.

Kipindi kilikuwa cha takriban saa moja na nilieleza maisha ya Karume kuanzia mwaka 1955 alipohudhurua mkutano wa kwanza wa TANU uliofanyika Ukumbi wa Hindu Mandal Dar es Salaam ambako alikutana na Mwalimu Nyerere na Karume akamualika Nyerere Zanzibar.

Nilieleza pia kuwa hiyo haikuwa ndiyo mwanzo wa kukutana.

Walikutana kabla Zanzibar Nyerere aliongozana na Abdul Sykes na Dossa Aziz ambao walikwenda kumtambulisha kwa Karume Rais wa African Association.

Mtangazaji wa AZAM TV Irene Kilenga alivutiwa sana na jina nililompa Mzee Karume - "The Mastermind," na alitaka kujua zaidi ni kipi kilinifanya mimi kumpa Mzee Karume jina hilo.

Nilimpa kisa chake toka mwanzo 1955 hadi kumalizikia kuuliwa kwake 1972.
Picha ya tatu ni ya Mkutano wa kwanza wa TANU mwaka wa 1955 uliofanyika Ukumbi wa Hindu Mandal, Dar es Salaam uliohudhuriwa na Abeid Amani Karume.











10Abdulkarim Ally, Hamisi Hababi and 8 others
 
Kumbu kumbu nzuri.Tupe kisa cha Master Mind
 
Back
Top Bottom