Azam Tv na janja janja za bei za vifurushi vipya

Azam Tv na janja janja za bei za vifurushi vipya

Makaoconset

New Member
Joined
Apr 20, 2012
Posts
2
Reaction score
2
Ni ukweli usiopingika hawa jamaa wana vipindi vizuri vinavyopendwa na watanzania walio wengi.Hata hivyo ujio wa king'amuzi kipya mwezi ujao pamoja na mambo mengine ulizinduliwa na "uwongo" wa kile kilichodaiwa kushusha bei ya malipo ya vifurushi kwa mwezi.

Hata hivyo, wakati nikiwasikiliza wakati ule, nilijiuliza swali la msingi, "Channels zilizokuwa zikioneshwa zitabaki vile vile?au wametumia NENO kushusha bei ya vifurushi halafu, 'bila kuwaambia wananchi' wahamishe channels za kifurushi kimoja kwenda kingine?Nikamuuliza mwenzangu akasema, HAPANA, "walichofanya ni kushusha bei za vifurushi ili kuwafanyia wepesi wananchi".

Sasa, leo nafungua TV yangu, nakutana na maelezo yafuatayo;

1.Channele zote za mpira zitapatikana kwenye kifurushi cha 20,000/= kuanzai dec 1!Mwanzoni ilikuwa 18,000/=, najiuliza AZAM TV wameshusha au wamepandisha?na kwa nini wawadanganye wananchi?

2.Azam 1 na Azam 2, zitapatikana kwenye kifurushi cha 13,000/=, zamani zilipatikana kwenye kifurushi cha 10,000/=, najiuliza wameshusha au wamepandisha? na kwa nini wawadanganje wananchi?

Hizi ni observations mbili nilizoziona, na sadly wametumia nguvu kubwa sana kuwaamninisha wananchi kwamba VIFURUSHI vimeshushwa na ukweli ni kwamba ni "UONGO",Huwenda wakawa na maana tofauti, ila nadhani WAMEWADANGANYA WANANCHI.
 
Guys kama kuna mtu anahitaji king'amuzi complete/full kit cha AZAM cha DISH ambacho ni kipya kabisa hakijamaliza hata mwezi na kimeshalipiwa chaneli zote kwa miezi mitatu. naomba anicheki DM tufanye biashara, kinapatikana kwa 165k (non-negotiable price)
 
Au kama kuna mtu ana king'amuzi cha DISH cha STARTIMES aje tubadilishane nimpe cha DISH cha AZAM but ataniongeza 60k ( NOTE: kingamuzi changu cha AZAM bado kipya hakijamaliza hata mwezi toka kinunuliwe na tayari kimeshalipiwa kwa muda wa miezi mitatu kwa chaneli zote )
 
Au kama kuna mtu ana king'amuzi cha DISH cha STARTIMES aje tubadilishane nimpe cha DISH cha AZAM but ataniongeza 60k ( NOTE: kingamuzi changu cha AZAM bado kipya hakijamaliza hata mwezi toka kinunuliwe na tayari kimeshalipiwa kwa muda wa miezi mitatu kwa chaneli zote )
Ingia DM mkuu

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom