Azam TV sio kila mteja wenu ni islamic

Acha chokochoko, mbona uwa hulalamiki zile tamthilia za South America zilizojaa ukatoliki na mapadri ambazo uwa zinarushwa sana sehemu nyingine bila kusahau zile za Kifilipino
Amepaniki tu
 
Wacha kutuletea udini wako hapa! Anzisha tv yako halafu weka vipindi unavyotaka wewe.
 
Ni kweli maudhui makuu ya tamthilia ya sultani ni kulingania dini ya kiislam na kuonyesha umma kwamba imani hiyo ni suprime over all others including Jewish and christianity
 
Anzisha yako
 
Wee angalia tu tamthilia hizo hizo, shida iko wapi! Mbona hata vingamuzi vingine tunakomaa tu na tamthilia full ukristo, na hakuna anayelalamika. Ushawahi ona Muislam analalamikia DSTV au ving'amuzi vingine au channel yoyote kuonesha tamthilia zenye maudhui ya dini za kikristo? Na ndio zilizoenea kuliko za kiislam. Mimi nakushauri ujikaze tu, au kimya kimya pambana na hali yako( hamia mtaa wa pili) lkn kulalamika hakutakusaidia chochote.

Shida ni kwamba tumezoea kuona hizo zenye maudhui ya kikristo sasa hizi nyingine zinatusumbua.

Hii pia imejengeka hata katika ofisi za umma au zozote, taasisi ikiongozwa na muislam hata wakiwepo waislam wachache na wakristo wengi wapo, lazima wakristo watalalamika wanasahau ofisi karibu asilimia tisini wamejaa wao tu, akili yako inakataa kuona mabadiliko, cha msingi kubaliana pia na vitu vingine, kubali akili iingize kitu kipya ndugu, sio kila siku kwaya na movie zinazoishia na maombi tu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
mi situmii hicho kisimbuzi kimekaa kidini dini...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Dstv
Kuna startimes
Kuna continental
Sio lazima utumie Azam decoder

Balance shobo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu inawezekana nikawa na kisimbuz cha dstv na startimes nikiwa na dish la strtimes??

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes inawezekana hata kama Transponder zao ni tofauti.

Mimi nina Dish la Zuku na satellite yao ni tofauti na Azam ila nikichomeka king'amuzi cha Azam naangalia vizuri tu.
 
Kuna kuna kipindi kulikuwa na malalamiko waigizaji wa uhuru ni waislam watupu, hawa azam ni wadini sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…