Sodoku
JF-Expert Member
- Feb 3, 2016
- 1,271
- 2,903
Hawa wadada wanaopokea simu zetu kutusaidia matatizo mbalimbali ya decoder za azam kiukweli waliopo azam wanasikitisha sana. Wadada hawa wanapokea simu kama vile hawataki kuzungumza na mteja. Hawaonekani kama wana tabasamu au wanaipenda kazi yao.
Unaongea na mdada anakukatisha au anamalizia maneno yako, yaani anaonesha hataki kuendelea kukusikiliza au ana haraka. Viongozi/human resource tafadhali angalia watu wako. Kiukweli ni dada mmoja tu ndiye aliwahi kunipa ushirikiano mzuri nami nikaona amenijali kama mteja. Lakini kabla ya hapo nilishaongea na wadada kama 3 wote wakiongea kama vile wanakereka na mteja wakati huo huo nyuma kukisikika watu wengine wanapiga story na kubishana.
Katika ulimwengu huu wa ushindani wa kibiashara mteja ni mfalme, mteja ni mume. Mtujali wateja wenu tunapokuwa na matatizo.