Azam Tv Wydad Casablanca FC watumiize Vichwa na Nyie tena? Muda kamili wa Mechi Morocco ni Saa ngapi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kwenye Kurasa zenu mmeweka Saa 4 Kamili, Mratibu wa Simba SC Abbas Ally jana katika Mahojiano na Vyombo vya Habari vya Tanzania kasema ni Saa 3 na siyo Saa 4 kama ilivyotangazwa awali, Leo Asubuhi Mtangazaji wenu wa Morning Express kasema ni Saa 3 na Watangazaji na Wachambuzi wa Kipindi chenu cha Michezo cha Jioni wanajichanganya mara waseme Saa 4 mara Saa 3 huku Redio nazo EFM, Clouds, Wasafi FM East Africa Radio nao wakishindana katika Kubahatisha muda Kamili wa Mechi ya Wydad Casablanca FC na Simba SC huko nchini Morocco.

Kiukweli mnatuchanganya mno yaani tuwaze Ugumu wa Mechi hii ya Leo na huku tena hata hatujui na hatuna uhakika wa muda Kamili wa Mechi kuanza.

Tafadhali semeni muda Kamili wa Kick Off ya hi Mechi vinginevyo taratibu sasa nami GENTAMYCINE nitaanza Kuwadharau na Kuwapuuza.
 
Kama Azam wanakuchanganya basi nenda kwenye kurasa za kimtandao za Wydad uangalie Wanasema saa ngapi!?
 
Unaumiza kichwa cha nini kisa Simba? We kaa kwa kutulia mpigwe subiri highlights uone vituko vya Onyango huku akifokewa na na kaka yake Ally Salum.

Huku kwenye bench Robertinyo anamnong'oneza Kibu kama mmeshindwa tukimbie tu. Pamoja na yote bado unataka ushuhudie hizi aibu zote?
 
wapumbavu hao Azam game iliyopita walikata chaneli.

sitaki kulifananisha na issue za siasa, ila naona kama kuna watu wameanza kuvimba kichwa sana
 
Nimeshaandaa nyimbo za kuanikiza mazishi wajameni๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿคฃ๐Ÿƒ๐Ÿƒ
Hivi huwa hupati Notification Exy jana nilikuita, kwenye uzi mmoja hukutokea.
 
Reactions: Exy
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ