Azam wanavuna walichopanda

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kuna wachezaji ambao hawana na mapenzi na Azam lakini wamewalazimisha kubaki kucheza Azam. Wachezaji hawa baadhi Yao wamewafungia kwa kisingizio Cha utovu wa nidhamu.

Ukweli ni kwamba club zisiwababinie wachezaji wanaotaka kuondoka hata kama wanaenda kwenye timu ambazo viongozi hawazipendi.
 
Huwezi kujenga timu isiyo na nidhamu
 
Azam wanapotezwa na wachezaji wenye Uyanga yanga.
Baada ya kuwaza mafanikio ya timu yao Azam.
Wanaiwazia Yanga
Na Yanga yenyewe ndio hivyo tena.
Inaupiga mwingi sana mechi za matopeni.
Na dhidi ya Simba basi.
 
Azam wana hela ila wanachemka sana kwenye usajili
 
Azam ilibidi waendeleze lengo lao la kukuza vipaji wawalee vijana wao kutoka chini mpaka timu kubwa.
Tatizo lao wameacha malengo yao na kutaka kushindana na Simba na Yanga.
 
Azam ilibidi waendeleze lengo lao la kukuza vipaji wawalee vijana wao kutoka chini mpaka timu kubwa.
Tatizo lao wameacha malengo yao na kutaka kushindana na Simba na Yanga.
Timu ya mpira ya Azam ni hovyo sana. Sasa walikuwa na ulazima gani wakuwapeleka mkopo vijana wao kama Tapes Evans,Oscar Masai na wengine kama lengo lao ni kubaki kupambania namba tatu kwenye ligi.Sioni sababu ya kusajili foreign players kama Mbombo ambaye five clear chances of scoring a goal anachofanya zero.
 
Niliwashangaa sana azam kuwaza makolo wachezaji wote wale
 
Utopolo wanachekesha kwa hiyo stahili ndio mnataka mpewe sureboy bure
Wabaki nae, mchezaji sio kama kuku kwamba unaweza kumfungia bandani atake asitake. Mbape kaamua hataki kubaki PSG lazima ataondoka TU, Pogba hataki Man U, Harry Cane hataki Tottenham. Kwanini Sureboy lazima acheze Azam au vinginevyo aende Simba?
 
Kama utaratibu ndio huo aidhani Kama yanga wangehangaika na Morison Hadi CAS maana Morison Hana mapenzi na yanga kwanini wanamlazimisha
 
Kama utaratibu ndio huo aidhani Kama yanga wangehangaika na Morison Hadi CAS maana Morison Hana mapenzi na yanga kwanini wanamlazimisha
Yanga haimtaki Morrison lakini viongozi wa Yanga hawataki kuamini kuwa Morison hakuwa na mkataba, ndiyo maana walikwenda cas. Kwakuwa viongozi walikuwa na kesi ya kudanganya mashabiki wa Yanga kuwa waliwadanganya, ndio maana wakakimbilia cas kujiosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…