Azam yapata hasara baada ya mechi kusogezwa mbele

Kamugisha138

Member
Joined
May 5, 2023
Posts
22
Reaction score
23
"Tumepata athari ya kifedha baada ya mchezo (dhidi ya Simba Sc) kusogezwa mbele, kwa sababu mchezo kama ungechezwa tarehe 6 kama ilivyopangwa basi tarehe 7 tungerudi na hivyo watu wangepumzika na kusingekuwa na haja ya watu kukaa kambini kuwahudumia."

"Lakini wametuongezea siku moja mbele ambayo sisi haikuwepo kwenye ratiba, hivyo muda wa maandalizi na kukaa kambini umeongezeka, na hivyo tumepata hasara kutokana na kuwahudumia watu siku hiyo wakiwa kambini," amesema Zakazakazi Afisa habari wa klabu ya Azam FC
 
Hawa wa upande wa pili wao hasara hawajapata? (Simba)
Sasa hapo ndo nashidwa kuelewa kwasababu
Muda waliopanga wa mechi ulivyosogezwa wamesema wanatumia ghrama kuhudumia na kulonge wachezaji wako maana wao ndo waliotangulia nangwanda sijaona huko mtwara
 
Hawa wa upande wa pili wao hasara hawajapata? (Simba)
Wa upande wa pili wameomba wao mchezo kusogezwa mbele ili wapate nafasi ya kukaa sawa kisaikolojia.
Au hata kama ingekuwa sivyo hivyo, kawaida mtu analia "mama angu wee" halii "mama etu wee" na hivyo ndivyo AZAM alivyolia.
 
Mantiki ya kuahirisha hii mechi ni nini au kwa vile ya Yanga iliahirishwa?
Hata mimi mwenyewe nimeshangaa! Sababu ya kuahirisha mechi ya Yanga vs SBS, walau ilikuwa na mashiko.

Sasa hii ya kuahirisha mechi ya simba vs Azam! Inashangaza kwa kweli.
 
simba wanaogopa kulowa hapo kwanza wanashiriki nini kingine mpaka mechi isogezwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…