Imepita muda sasa Azamtv kupitia online app yenu mmeitoa channel ya azamsport, hivi karibuni pia mmeitoa ZBC2. Kwa kweli mnaumiza walio nje ya nchi maana ndio mlikuwa faraja yetu hasa kwa wapenzi wa ligi ya nyumbani hata mechi za kimataifa kwa klabu zetu pendwa na timu yetu ya taifa.
Kuna kipindi nilisikia kuwa hamkuwa na kibali cha kurusha hizo channel nje ya nchi, mkasema mtashughulikia lakini kimya mpaka leo. Nadhani mnatakiwa kuongeza jitihada maana mlifika level ya juu kuliko ving'amuzi vingi Tanzania kwa kupatikana duniani bila chenga .