Azimio la Balfour(1917): Ushahidi wa kuporwa ardhi ya Palestina

Azimio la Balfour(1917): Ushahidi wa kuporwa ardhi ya Palestina

Joined
Nov 23, 2018
Posts
94
Reaction score
202
Azimio la Balfour lilikuwa ni taarifa ya umma iliyotolewa na serikali ya Uingereza mwaka 1917 wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia ikitangaza kuunga mkono harakati za Shirika la Kizayuni kuanzishwa kwa taifa la Kiyahudi katika ardhi ya Palestina. Ikumbukwe Uingereza wakati huo ilikuwa "super power" hivyo Isingekuwa rahisi Kwa mpango huu kushindikana.

Tamko hilo lilikuwa katika barua ya tarehe 2 Novemba, 1917 kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza 𝗔𝗿𝘁𝗵𝘂𝗿 𝗕𝗮𝗹𝗳𝗼𝘂𝗿 kwenda kwa Lord Rothschild, kiongozi wa jumuiya ya Kizayuni ya Uingereza.

Barua halisi kutoka kwa Balfour kwenda kwa Rothschild inasomeka:

"Serikali ya mtukufu ina muono wa kuunga mkono kuanzishwa makazi ya kitaifa ya Wayahudi katika Palestina na itatumia juhudi zao zote kuwezesha kufikiwa kwa lengo hili, inafahamika wazi kwamba hakuna kitakachofanyika ambacho kinaweza kuathiri haki za kiraia na kidini za wanajumuiya wengine wasio Wayahudi waliopo Palestina, au haki na hadhi ya kisiasa inayofurahiwa na Wayahudi katika nchi nyingine yoyote."

𝗠𝘆 𝘁𝗮𝗸𝗲
Barua ya Balfour kwa Rothschild inatoa hoja ya utetezi juu ya uhalali wa vuguvugu la Wapalestina kudai ardhi ya mababu zao kwakuwa Israeli imeundwa isivyo halali kwenye nchi ya Palestina. Sehemu ya Azimio la Balfour inasema:

"His Majesty's Government view with favour the establishment 𝗶𝗻 𝗣𝗮𝗹𝗲𝘀𝘁𝗶𝗻𝗲 a national home for the Jewish people.."

Kwa msingi huo, naamini ipo siku Wapalestina watapata haki yao kwani daima haki hushinda dhuluma.
Balfour_declaration_unmarked.jpg
 
Back
Top Bottom