Maalim Raphael
Member
- Nov 23, 2018
- 94
- 202
Azimio la Balfour lilikuwa ni taarifa ya umma iliyotolewa na serikali ya Uingereza mwaka 1917 wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia ikitangaza kuunga mkono harakati za Shirika la Kizayuni kuanzishwa kwa taifa la Kiyahudi katika ardhi ya Palestina. Ikumbukwe Uingereza wakati huo ilikuwa "super power" hivyo Isingekuwa rahisi Kwa mpango huu kushindikana.
Tamko hilo lilikuwa katika barua ya tarehe 2 Novemba, 1917 kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza ๐๐ฟ๐๐ต๐๐ฟ ๐๐ฎ๐น๐ณ๐ผ๐๐ฟ kwenda kwa Lord Rothschild, kiongozi wa jumuiya ya Kizayuni ya Uingereza.
Barua halisi kutoka kwa Balfour kwenda kwa Rothschild inasomeka:
"Serikali ya mtukufu ina muono wa kuunga mkono kuanzishwa makazi ya kitaifa ya Wayahudi katika Palestina na itatumia juhudi zao zote kuwezesha kufikiwa kwa lengo hili, inafahamika wazi kwamba hakuna kitakachofanyika ambacho kinaweza kuathiri haki za kiraia na kidini za wanajumuiya wengine wasio Wayahudi waliopo Palestina, au haki na hadhi ya kisiasa inayofurahiwa na Wayahudi katika nchi nyingine yoyote."
๐ ๐ ๐๐ฎ๐ธ๐ฒ
Barua ya Balfour kwa Rothschild inatoa hoja ya utetezi juu ya uhalali wa vuguvugu la Wapalestina kudai ardhi ya mababu zao kwakuwa Israeli imeundwa isivyo halali kwenye nchi ya Palestina. Sehemu ya Azimio la Balfour inasema:
"His Majesty's Government view with favour the establishment ๐ถ๐ป ๐ฃ๐ฎ๐น๐ฒ๐๐๐ถ๐ป๐ฒ a national home for the Jewish people.."
Kwa msingi huo, naamini ipo siku Wapalestina watapata haki yao kwani daima haki hushinda dhuluma.