Smart codetz
JF-Expert Member
- Jan 25, 2023
- 218
- 875
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga ya Dares Salaam, Stephane Aziz Ki amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Aprili wa Ligi Kuu ya NBC huku Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Abdallah Mohammed, akichaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo.
Kikao cha Kamati ya Tuzo za TFF kilichokutana Dares Salaam Jumamosi Mei 6, kilimchagua Ki, baada ya kuonesha kiwango kizuri kwa mwezi Aprili na kutoa mchango mkubwa kwa Yanga, ikiwa ni pamoja na kufunga mabao matatu katika dakika 135 alizocheza kwa michezo miwili akiwa na Yanga.