kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Nianze kwa kusema hata mimi nauona mwanga kwenye kuwekeza kwenye kilimo chenye tija kutokana na ukubwa wa nchi yetu yenye kila kitu kinachofaa kwa kilimo, ufugaji na uvuvi.
Hofu yangu kuu kuhusu huu mkakati wa Waziri Bashe na Rais Samia wa block farming nauna kama vile hauna tofauti na ule wa awamu ya nne wa Kilimo kwanza na hata ile kilimo ni uti wa mgongo, siasa ni kilimo, nk ya awamu zilizopita. Awamu ya tano iliachana na kilimo na ikajikita kwenye viwanda kwanza.
Maswali ya msingi ni
1. Je, Block farming inatofautianaje na ile mikakati mingine iliyopita ya CCM ambayo haijazaa matunda?
2. Je, block famining ni ajenda ya kitaifa au ya CCM tena CCM ya awamu ya sita tu?
3. Hivi tuna uhakika gani kama awamu zote za uongozi wa CCM na hata vyama vya upinzani kama vikishinda uchaguzi block farming itapewa kipaumbele?
4. Kwa ajili ya kampeni tu?
Nijuavyo mimi kilimo ni lazima kiwe ni agenda kubalifu kwa wadau wote nchini kuwa huu ndio mwelekeo wetu kama taifa. Na mwelekeo huu unapaswa kuanza na kuyapima na kuyatambua maeneo yote ya kilimo, ufugaji na uvuvi nchi nzima ili maeneo hayo yasibadilishiwe matumizi milele na milele.
Pili kujenga maabara za udogo kwa kila wilaya kama sio kwa kila kata, tatu kujenga maghala ya kuhifadhia mazao husika kila kijiji/kata na kujenga barabara kabla hata watu hawajalima chochote, na nne kuyatambua masoko ya mazao husika kabla watu hawajaanza hata kulima chochote. Kuanza kulima kabla ya kujibu maswali haya kabla ni sawa na kutanguliza mkokoteni mbele ya punda.