Foul
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 796
- 1,160
Kuna mambo fikirishi kidogo, kwamba Wakenya wanakuja Tanzania wananunua mazao, mathalani Mahindi, vitungu hata matunda yakiwemo Machungwa na Parachichi (Hass Ovacado), lakini kilio kikubwa na hata ugomvi wetu na majirani zetu hawa chanzo kimekuwa Mahindi, nasema ni Mahindi maana sijawahi sikia ugomvi wetu na Rwanda kisa muhogo kutoka Kigoma unaenda huko au mpaka kufungwa ili Muhogo usiende Rwanda au Burundi
Si mara moja Serikali yetu imepiga marufuku kuuza Mahindi nje ya nchi, ili kuzuia ukosefu wa chakula, sina hakika sana kama Mahindi ndo chakula pekee kikikosekana basi Nchi nzima inazama kwenye Baa la njaa, labda ni kweli maana Waafrika utawatengenishaje na Mahindi? Hapa Tanzania najua ndo chakula kikuu kwa familia nyingi, sisemi zile kaya Maskini tu, hata Matajiri japo si mara nyingi, lazima wale ugali
Kwahiyo, mara zote Serikali imekuwa ikipiga marufuku uuzaji wa Mahindi hayo nje ya nchi pale inapoona uzalishaji ulikuwa mdogo, lakini mwaka huu pamoja na uzalishaji kuwa mdogo kuliko miaka mingine kutokana na Uhaba wa mvua, hali ya hewa hapa imechangia, Serikali kupitia Waziri wa Wizara ya Kilimo Mh. Husein Bashe imesema haitozuia mahindi kwenda popote, na anayeona Mahindi ni ghali basi akalime, mie namuunga mkono kwa 100%
Lakini kuiunga mkono Serikali katika hili haimaanishi hakuna ambacho walipaswa kufanya, kuna jukumu ambalo Serikali haijalifanya sawa sawa na kama ikilifanya, hutosikia kilio cha kwanini Mahindi yaende Kenya
Kwanza lazima tukubaliane, yeyote anayeweka fedha yake shambani, anatafuta faida, kuna kitu kimoja kinawasumbua watu, "Mazao ya Biashara na Mazao ya Chakula", watu wanadhani kwa kuwa Mahindi ni miongoni mwa mazao ya chakula, basi si zao la biashara, huku ni kutokuelewa mantiki ya kwanini tuliita 'mazao ya biashara na mazao ya chakula", au pia ni kutokujua historia ya kwanini tuliyaita hivyo wakati huo, hilo andiko lingine, lakini hapa nitaeleza kidogo kuwa kila zao ni zao la biashara, tofauti ni matumizi tu
Mfano, Katani huwezi kula, lakini mahindi utakula, na yote utayafanyia biashara, huwezi kumzuia Mkulima aliyechukua Milion zake 10 akaweka shambani eti asiuze penye bei nzuri Mahindi yake maana nchi itaingia kwenye njaa, vyakula vitapanda bei, huu ni ujinga na ni sababu nyingine ya kuuchukia Ujamaa, maana kama ni kwa ajili ya kula, mtu si atalima nusu Heka yake, mahindi yanayomtosha yeye na familia yake? Ya nini alime Heka 20 wakati familia yake itashiba mwaka mzima akilima nusu Heka? Ujamaa unadumaza uzalishaji
Basi, Serikali inapaswa kufanya nini? Kwanza kabisa Serikali inatakiwa itumie vyombo vyake vyema kabisa, Ujasusi wa Kiuchumi hapa ulipaswa utumike haswa, kwanza kama serikali ikiweka nguvu kwenye hili zao la Mahindi, basi umaskini utapungua sana kwa Wananchi wake maana soko tayari tunalo, ni kitu gani tena tunataka? Namkumbuka Mzee wa Fursa, Maremu Ruge (Mungu amuweke sehemu salama) kwamba 'anzia Sokoni', jua soko linataka nini na kwa kiasi gani ndipo urudi kuzalisha au kusambaza,Tushajua Kenya wanatutegemea kwa Mahindi, Sudan kusini na Congo DR vilevile, kwanini tusiwekeze nguvu kubwa kwa wananchi, tulime kwa ukubwa, tuwalishe wote, nchi ipate fedha na wananchi watoke kwenye Umaskini?
UJASUSI WA KIUCHUMI
Tulipaswa kama nchi tujue Kenya na hizo nchi nyingine zinazohitaji Mahindi kutoka kwetu, watahitaji kiasi gani? Wala si kazi sana maana kila nchi hutoa takwimu zao, Mategemeo ya mahitaji yao na uwezo wa bei wanaoweza kulipa watumiaji au wanachi wao (Comsumer Price Index), na taarifa nyingine za kufanana na hizo, kwahiyo nchi itaangalia mahitaji yetu, na makadirio ya chakula kilichozalishwa, kama tukiona makadirio yetu na mahitaji yetu na ya nchi jirani na makadirio ya uzalishaji yanawiana, tunaacha Soko liamue cha kufanya
Ikiwa tumeona uzalishaji ni mdogo kwa kulinganisha na mahitaji yetu na ya majirani ( mara nyingi hapa ndipo Serikali hukosea kwa kupiga marufuku mahindi kuuzwa nje ya nchi kwa kufunga mipaka) basi ndipo Maghala ya chakula yatumike, nitaeleza kwa kirefu kidogo hapa
Tunayo maghala ya chakula ya Serikali, Serikali ikiona tatizo hilo la uhaba litatokea, basi serikali inunue mahindi kwa bei ya ushindani iliyopo sokoni, kama Kenya wananunua Gunia la Kilo 90 kwa Tsh 75,000, basi serikali inunue kwa bei hiyo au iongeze kidogo maana gharama za usafirisha hazitakuwa kubwa kama wale watakaopeleka Kenya, ihifadhi kwenye hayo Maghala ya chakula ya Serikali
Serikali ikishafikisha kile kiasi ambacho kwa makadirio yao inaona itatosha kwa mwaka mzima, basi inasubiri ifike kile kipindi ambacho kuna uhaba mkubwa kabisa, wakati ambao wanaona kuna mfumuko wa bei usio wa kawaida, wale wafanyabiashara walionunua Mahindi na kuhifadhi ili waje wauze bei ikiwa kubwa wanapata faida kubwa kuliko (Supper Normal Profit), na kusababisha mfumuko wa bei usio himilivu, basi Serikali inapeleka mahindi sokoni kupunguza uhaba
Sisemi Serikali iwape wananchi chakula bure, wala haitaweza, unaipa Kaya moja yenye watu 7 kilo 90 za mahindi, watakula kwa muda gani? Alafu ni bora hizo kilo 90 zingeenda kama Serikali ilivyokusudia, Mnawajua watendaji wa Vijiji na Kata nyie? Tena wanashirikiana na Wakurugenzi kabisa, Kaya moja itapata kilo 10 mpaka 20, mengine mnaambiwa watayapekeka shuleni, uongo mtupu, hilo nimeshuhudia kwa macho yangu enzi za Kikwete, tuachane na hayo
Kuna sababu moja tu itafanya bidhaa ipande bei, Uzalishaji/usambazaji (Supply) ukiwa mdogo kuliko mahitaji (Demand), kwahiyo Serikali itakachofanya ni kuongeza usambazaji ili angalau ipunguze umbali kati ya Uhitaji na Usamabazaji (Demand and Supply)
Kwa kufanya hivyo, Serikali itakuwa imezuia mfumuko wa bei bila kugombana na raia, wala wafanyabiashara, na fedha iliyotumika kununulia hayo mahindi kwa mfano itarudi tena na faida kidogo, kwa kuwa lengo la Serikali si kufanya biashara, basi isilenge faida bali ongezeko kidogo la mtaji ili kulinda thamani ya hiyo fedha, hiyo faida kidogo ndiyo itakuwa kwa ajili hiyo ya kulinda thamani ya hiyo fedha, inachopaswa kufanya Serikali, ni kujizuia kuzidisha Usambazaji (Supply) kuliko Mahitaji (Demand) maana itafanya bei iwe chini na itaua mitaji ya wafanyabiashara wake
KILIMO BIASHARA (AGRIBUSINESS)
Hakuna mtu ambaye kwa sasa hajui kuwa Kilimo ni biashara, bila kujali unalima zao gani, zamani kwa mfano watu walilima Magimbi kwa ajili ya familia zao tu, siku hizi wanalima kwa ajili ya biashara, Mihogo, Viazi vitamu, Pilipili na mazao yote kwa ujumla wake, na yeyote atakaye fanya biashara hii anategemea faida, sawa na wewe uliyefungua duka la vyombo vya mziki, au Soloon au Bar ili tuumwagilie moyo
Kwahiyo, hata kama ni wewe unayetamani Serikali ipige marufuku kuuza Mahindi Kenya, basi lazima ungeuza penye bei nzuri, ili upate faida,
Kuna hoja kwamba, wanaofaidika na bei kubwa sio wakulima bali wafanyabiashara na Madalali wa mazao, lakini mie nakuuliza wewe hapo, ni biashara gani inatoka kwa mzalishaji na kwenda kwa mlaji wa mwisho moja kwa moja? Tena ifanyike kwa ukubwa, ni ipi? Unataka kama mahindi Kilo 1 inauzwa 1000Tsh basi mkulima achukue yote? Lazima kuwe na mnyororo wa watu, Mawakala, Madalali na wengineo, ambacho kinapaswa kifanyike ni Serikali ihakikishe wakulima hasa wadogo maana ndo hunyonywa zaidi wapate taarifa za kinachoendelea Sokoni, taarifa zitoke mara kwa mara kupitia radio zetu hasa ya Taifa na taarifa hizo zitoke kwa uzito na msisitizo, mwananchi Mkulima, akijua gunia la Mahindi la kilo 90 ni 80,000tsh huko sokoni, hawezi kulaghaiwa na dalali eti ampe elfu 35 tu, hatokubali
Kingine ni kuwaambia kwa msisitizo, wakulima waunde vyama vya ushirika wa mazao ya Kilimo na Masoko (AMCOS) ili wauze mahindi yao kwa pamoja kuliko kuuza mmoja mmoja, hii inapunguza ulaghai, lakini pamoja na kuunda vyama hivyo vya ushirika, suala la taarifa ya bei Sokoni ni Muhimu maana vyama vyenyewe wanajaa wezi
HITIMISHO
Ikiwa tunataka kweli kama taifa tuongeze uzalishaji, tuondoe kabisa suala la uingiliaji wa serikali (Gvt interaction) hasa hili la kuingilia kuzuia (Block) badala ya kuhamasisha, kazi ya serikali iwe ni kusimimia ili tupate bidhaa bora na si kupiga marufuku, hii ya kupiga marufuku kwenye jambo lolote ni kuzuia ubunifu, Wenzetu Wa ulaya wangekuwa ni watu wa kupiga marufuku, wasingetengeneza hata baiskeli,
Kwenye suala la kilimo mathalani, ili uzalishaji uwe mkubwa, ni lazima soko lililopo lilindwe na liongezwe, unaweza kutolea mfano zao la Mbaazu lililokufa kifo cha Mende baada ya soko lake kufa na yote ilitokana na sera mbovu za Serikali, hata Mahindi yasingekuwa ni chakula kikuu huku kwetu, leo kulimo cha zao hili kingekuwa shakani kutoka na kuzuia mipaka mara kwa mara wakulima wanapopata mavuno machache, wakati huo ndio ungekuwa muda wa kurudisha gharama zao kubwa walizotumia alafu wakapata mavuno machache kutokana na mvua kuwa chache
Yaan watu wamepata hasara, alafu unawazidishia hasara kwa kuwazuia kuuza penye bei nzuri? Hii ni HAPANA kubwa

Upvote
0