A
Anonymous
Guest
Wapangaji wa Shirika la Nyumba zilizopo karibu na Manispaa ya Morogoro tunalalamika bar maarufu ya Ellis iliyopo karibu na Ofisi za Manispaa ya Morogoro, inapiga kupiga mziki mkubwa hadi asubuhi hali ambayo ni kero kubwa kwetu.
Sisi Wapangaji baadhi ni Viongozi na Watumishi wa Umma tuliwasilisha malalamiko yetu kwa kwa NEMC, siku za nyuma na yalifanyiwa kazi lakini kwa sasa changamoto hiyo imerejea tena, tunaomba Serikali kuingilia kati.
Inawezekana kuna mkubwa yupo nyuma ya hiyo bar na ndio maana wahusika wamekuwa wakivunja Sheria mara kwa mara na hakuna hatua zinazo chukuliwa ikizingatiwa kuwa jirani na ofisi za umma.
Nyakati za usiku kuna wakina dada wanaojiuza lakini pia wapo wanaume mashoga ambao hapo ndio kama eneo lao maarufu la kukutana na wateja wao.
Ushauri.
Ni vizuri biashara zinazoendelea hapo zikafuatiliwa kwa ukaribu kwakuwa eneo hilo lipo karibu na ofisi za umma haitapendeza kuona biashara ya ngono zikifanyika katika eneo hilo.
Pia Manispaa ya Morogoro ni vizuri ikaweka taa zenye mwanga mkali katika eneo lote la uzio ili kuondoa giza katika eneo hilo kuzuia kuwepo kwa biashara yoyote.
Ufafanuzi wa NEMC ~ NEMC: Tunachunguza madai ya Baa ya Ellis kuwa imekuwa kero kwa majirani kutokana na kelele za muziki