Siasa Tanzania zilivyo pamoja na ukweli kuwa Mara zote Lipumba na wenzake wamekua wakiiunga mkono CCM kwenye uchaguzi mkuu hasa upande wa Urais lakini bila kuondoa ubinafsi wa Mbowe na uroho wa madaraka pamoja na mwenzake Lipumba na kuunganisha nguvu za vyama hivi viwili pamoja na Kile cha ACT kamwe wapinzani hawataingia madarakani hata pakiwa na time huru na katiba mpya na mahakama huru kabisa.
Chadema chenyewe hakiwezi kuishinda CCM na CUF yenyewe haiwezi kuishinda CCM. Lakini CUF kikishirikiana na Chadema na vyama vingine kinaweza kwa hakika kuiangusha CCM kwa kishindo kikubwa.
Kilichopo ni kwamba Viongozi wa vyama hivi ni makada wa CCM waliopo upinzani kwa ajili ya maslahi yao. Hawana mpango wa kuiondoa CCM madarakani ndio maana kila mmoja hayupo radhi kuona miongoni mwa vyama vya upinzani kinaingia ikulu. Wanajua kuwa CCM ndiye aliyewaweka kwa kazi maalum na hawataki CCM iangushwe mana ikiangushwa basi dili lao litakua limekwisha ndani ya upinzani.
Hua najiuliza kama mtesi wa upinzani ni CCM inakuaje Chadema au CUF au ACT wanashindwa kuungana hata kama wana tofauti zao za kisiasa.
Tofauti ya CUF na Chadema kwa mtizamo wangu haiwezi kuwa ni sababu ya kujenga uadui mkubwa na kuona bora CCM ishinde wakati wako madarakani miaka nenda rudi.
Wapinzani wangemjua adui na mshindani wao anayetumia mbinu zozote kupata ushindi basi wangekua wanapeana kampani kwenye uchaguzi.