Mrema David
Member
- Jul 19, 2022
- 5
- 3
Ahsante kocha Nabi! Ahsante Bernard Morrison! Ahsante Jonas Mkude! Ahsante Kali Ongala! Ahsante Abdallah Shaibu! Ahsante Erasto Nyoni! Ahsante Cleophace Mkandala! Ahsante Dickson Ambundo! Ahsante Beno Kakolanya! Ahsante Nelson Okwa! Ahsante Agrey Moris! Ahsante Mahamoud Mroville! Ahsante Bruce Kangwa, Tuisila Kisinda, Gadiel Michael…na kuendelea.
Ni utamaduni na haiba yetu, na pia ni kuonesha heshima, kujali, na kuthamini mchango wa mtu mwingine katika maisha yako kwa kusema AHSANTE. Mlolongo wa AHSANTE tuliouona na tunaoendelea kuuona na tutaendelea kuuona katika klabu zetu, kwa lugha rahisi ni kutoa mkono wa kwaheri kwa wachezaji, makocha, na watendaji wengine baada ya huduma yao kwa kipindi fulani na kuwashukuru kwa mchango walioutoa katika klabu husika.
Lakini pia AHSANTE hii imebeba maana tofauti tofauti kwa walioagwa. Kuna ambao wameagwa kwa sababu za kimaslahi, kuna walioagwa kwa sababu ya viwango vyao kutokidhi mahitaji ya klabu au uwezo wao kuwa chini ya matarajio ya klabu, na kuna walioagwa kwa sababu ya muda wao wa utumishi ndani ya klabu husika kufikia tamati
Eneo la maslahi linagusa moja kwa moja mikataba. Kadri muda unavyokwenda, thamani ya mchezaji au kocha inaweza kupanda au kushuka kulingana na kiwango chake. Timu inaposaini mkataba na mchezaji au kocha, inajifunga naye kwa muda fulani kwa kwa matarajio fulani. Unaweza kumnunua mchezaji kwa dau kubwa na kukubali kumlipa mshahara mkubwa, lakini asioneshe kiwango kinacholingana na thamani yake. Lakini pia timu inaweza kupata mchezaji kwa bei ndogo au ya kawaida tu na akaonesha kiwango kikubwa na kupanda thamani. Ishu ya kimaslahi inakuja vipi? Mvutano kati ya thamani na viwango ndio unaoleta migogoro ya kimaslahi. Mtu mwenye kiwango kikubwa lakini thamani ndogo anahisi kuonewa pale anapoona mtu mwenye kiwango cha chini anapewa thamani kubwa. Wakati mwingine viongozi wa vilabu wanashindwa kufanya maamuzi sahihi kutokana na presha ya baadhi ya wachezaji kuwa na majina makubwa au upendeleo unaotokana na kujuana. Mchezaji anapoona hapewi thamani anayostahili, anaona ni vema kuondoka na kwenda mahali anapoona atathaminiwa kulingana na kiwango chake. Mpira ni kazi; hawa wachezaji na makocha wana maisha pia. Hivyo maslahi mazuri ni kipengele muhimu cha kutazamwa kulingana na uwezo wao.
Aidha kuna nyakati zingine ambapo kunatokea ukiukwaji wa mikataba. Vipengele vya mkataba visipofuatwa, inaweza kuigharimu timu au mchezaji au mwalimu. Weledi mkubwa sana unahitajika katika kuhakikisha mikataba inatunzwa na kufuatwa vema ili kulinda taswira ya timu na wote wanaohusika.
Kuna wakati timu zinasajili wachezaji lakini wanapofika wanashindwa kukidhi mahitaji ya timu kwa msimu husika. Hapa lazima tuangalie mambo ya kuzingatia wakati wa kusajili:
-Je anaingia kwenye mfumo wa timu?
-Je anafiti kwenye malengo ya timu kwa kipindi husika?
-Je ana nidhamu? (nje na ndani ya uwanja)
Kuna wakati mchezaji anashindwa kufikia matarajio ya waajiri wake kwa sababu za kiufundi au kimaisha. Kuna wachezaji wenye viwango vikubwa lakini wanashindwa kuvionesha katika timu zingine kutokana na kutoingia kwenye mfumo wa timu, na wengine kupata majeraha ya muda mrefu hivyo kupelekea viwango kushuka. Lakini pia wengine wanashindwa kufikia matarajio kutokana na kukosa nidhamu kwa waajiri wao, kwa wapinzani, kwa mashabiki, au kwa mamlaka zinazosimamia michezo. Hii inaingia kwa benchi la ufundi pia. Timu inapoajiri kocha na wataalam mbalimbali kwenye eneo la ufundi, inatarajia matokeo chanya. Hivyo wachezaji na makocha wanaposhindwa kukidhi matarajio ya timu, ni hasara kwa timu husika.
Kuna wachezaji wanakaa kwenye timu kwa muda mrefu aghalabu miaka 10 na kuendelea, na hawa huachwa kwa heshima. Hivi karibuni tumeona klabu ya Simba ikimpa mkono wa kwaheri kiungo mwandamizi Jonas Gerald Mkude baada ya kudumu klabuni hapo kwa muda wa miaka 13. Wadau wengi wamehoji endapo Simba imeandaa tukio maalum kwa ajili ya kumuaga Mkude mbali na mitandaoni, kutokana na kuwa mchezaji ambaye amedumu Simba katika vipindi tofauti na katika hali zote. Bila shaka Mkude atapewa heshima anayostahili na klabu ya Simba. Tuwe watulivu na kusubiri kwani kipindi cha nyuma tuliona baadhi ya wachezaji wakiagwa katika siku maalum ya Simba.
Baada ya kutoa AHSANTE kwa wanaoondoka, ni vema kukaa chini na kuwaza MABORESHO kwa msimu ujao na zaidi. Kila timu inapaswa kuwa na malengo madhubuti kwa mashindano yaliyo mbeleni, na kuhakikisha wanapata watu sahihi wa kuwezesha malengo hayo kufikiwa. Kwa kutilia mkazo, klabu zetu zitakazotuwakilisha katika mashindano ya kimataifa ni vema kuwa na mikakati madhubuti ya kupata watu wa kiwango cha mashindano hayo. Wataalam wa skauti za wachezaji, makocha na majopo yao, pamoja na watendaji wakuu wa timu wafanye tathmini makini na kudadavua mahitaji ya timu kwa mashindano ya ndani na nje, na kujipanga kupambana vema na timu zingine ambazo zimekuwa zikifanya vizuri kimataifa. Tusisajili kwa mihemko, au kwa kushindana, au kwa majina; tusajili kwa tija, ili baadae hizi AHSANTE pia zioneshe tija.
Lakini katika kufanikisha hili, wafadhili na viongozi wa klabu pekee hawawezi. Kwenye andiko langu la GOLI LA MAMA, niliainisha kipengele cha uwekezaji. Wadau wa mpira wa miguu na wenye mapenzi mema na soka la Tanzania tuwe tayari kutoa mchango wetu wa aina yoyote ile ili kuhakikisha mafanikio, maana maboresho na mafanikio ni gharama.
Hali kadhalika, maslahi ya waajiriwa yaandaliwe vema na kuzingatiwa ili kuepusha migogoro mbalimbali. Tumeshuhudia baadhi ya kesi za wachezaji na klabu au makocha na klabu zinazopelekea wachezaji au makocha kutotimiza majukumu yao ipasavyo wanapokuwa bado ndani ya klabu, pamoja na kesi nyinginezo zinazoibuka baada ya wachezaji au makocha kuachana na klabu zao. Hii inapaswa kuepukwa kwani inaleta hali ya sintofahamu na upotevu wa rasilimali ambazo zinapaswa kutunzwa kwa manufaa ya timu.
Pia nidhamu za wachezaji na watendaji wote wa timu zitiliwe mkazo. Linapotokea tukio lolote la utovu wa nidhamu, kinachoharibika ni timu na sio mtu binafsi. Na ni vema kutambua kwamba, nidhamu bora inaleta mafanikio bora.
Kwa wachezaji walioagwa, maisha yanaweza kuendelea kwingine. Kulingana na viwango vyao, bado wana nafasi ya kuendeleza vipaji vyao. Kuna ambao wameshapata timu nyingine, mfano Erasto Nyoni aliyetimkia Namungo. Kwa wale walioacha alama njema, wapewe heshima yao, na kwa waliobaki waendeleze viwango bora na nidhamu ili baadae wapewe AHSANTE zisizo na mawaa.
Mwisho ninawaza kwa sauti: Baada ya sakata la Fei Toto na Yanga, je tutarajie “AHSANTE FEI TOTO” au hii imeenda?
AHSANTENI WAKUU,
AHSANTE TANZANIA.
Nawasilisha!

Attachments
-
Fei toto Azam fc (chanzo-azam fc instagram).jpg209.2 KB · Views: 3 -
Thank you Bernard (chanz0-yangasc instagram).jpg195 KB · Views: 4 -
Thank you Kali (chanzo-azam fc instagram).jpg265.1 KB · Views: 4 -
Thank you Mkude (chanzo-simbasc instagram).jpg150.4 KB · Views: 4 -
Thank you Mroville (chanzo-coastal union instagram).jpg187.9 KB · Views: 4 -
Welcome Nyoni (chanzo-namungo fc instagram).jpg104.8 KB · Views: 4
Upvote
1