Baada ya Bodi ya Filamu kumfungia Wema Sepetu, Chama cha Waigizaji Kinondoni nacho chamfungia

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Chama cha waigizaji mkoa wa Kinondoni (TDFAA) kimemfungia mwanachama wake Wema Sepetu kujihusisha na masuala ya filamu kwa muda wa miaka miwili.

Huo ni mwendelezo wa adhabu kwa mwigizaji huyo kufuatia kusambaa kwa video inayomuonyesha akifanya vitendo vinavyokinzana na maadili ya Mtanzania.

Chama hicho kimekwenda mbele zaidi na kutaka mamlaka za kiserikali zipuuze utetezi unaotolewa na mwigizaji huyo ambaye ni mrembo wa Tanzania mwaka 2006 kwa kuwa una lengo la kuvipumbaza visimchukulie hatua.

Msemaji wa chama hicho, Masoud Kaftany akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Oktoba 29, 2018 amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kamati ya maadili kujadili suala hilo kwa kina.

“Hii si mara ya kwanza kwa Wema kufanya mambo ya ajabu, aliwahi kuanika video ya makalio tukamuita akaomba radhi, safari hii ndio amefanya haya,’’ amesema Kaftany.

Amesema kamati imeunga mkono hatua zilizochukuliwa na bodi ya filamu na imeliomba Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kumuongezea adhabu itakayomzuia asijihusishe na shughuli zozote za sanaa kwa kipindi cha miaka miwili.

Katibu Msaidizi wa chama hicho, Herrieth Chumila amesema baada ya picha hizo kuanza kuzagaa walifanya jitihada za kumtafuta msanii huyo lakini hazikuzaa matunda.

“Tulimuita akasema yupo Burundi ila tunafahamu haikuwa kweli kana kwamba haitoshi leo pia tulimuita aje hapa lakini hajatokea,” amesema Chumila.

Chumila amesema kamati hiyo ipo macho kwa wasanii wake hivyo waache matendo yanayoweza kuchafua taswira ya sanaa na taifa kwa ujumla.

Chanzo; Mwananchi
 
Tanzania sijui kwanini swala la kujiamini hua ni mtihani sana kwetu, hawa mwanzo walikaa kimya kwenye matukio yote ya wasanii wa filamu waliopata sekeseke kama hili la video chafu, ila kwa hili la wema wamepata kujiamini kumfungia baada kuona tamko la serekali juu ya hilo swala.

Ila ushauri wangu kwa hawa wanaokurupuka kutoa matamko ya kumfungia watu hovyo bila hata ya kukaa chini na kumsikiliza upande wake ana utetezi gani dhidi ya tuhuma hio, kisha kuchanganua na ndio kutoa hukumu. Wana feli.

URT. Sheria ina sema, nanukuu,

Article 13) (1). "Kila mtu ana USAWA mbele ya sheria (vyombo vya sheria), bila ya ubaguzi wowote, kupewa ulinzi na haki mbele ya sheria"

Article 13) (6). "Kuhakikisha usawa mbele ya sheria/vyombo vya sheria, vyombo husika serekalini vinapaswa kuchukua hatua/njia sahihi ili kuhakikisha usawa huo unapatikana au kuchukua hatua zilizo ainishwa hapa chini;

Artile 13) (6) (b). Hakuna mtu anapaswa kutiwa hatiani mpaka itakapo thibitishwa na chombo husika ya kua ana hatia ya kutenda kosa la jinai......." NB HAPA kuna haki zinaitwa NATURAL JUSTICE (Haki za Asili) mtu ana haki ya kusikilizwa upande wake kuhusu utetezi, ana haki ya kutetewa/kuwakilishwa na mtu anaye ona anafaa kumwakilisha wakati wa kusikilizwa shauri hilo dhidi yake n.k.

Bila kufata haki hizo juu, basi hukumu zote zitakazo tolewa dhidi yake zitakua ni BATILI/HAZINA NGUVU mbele ya mahakama (akikata rufaa mahakamani dhidi ya hukumu za hivyo vyombo husika vilivomfungia/vilivyompa adhabu bila kumpa haki zake za asili, kama vile kumsikiliza/kupewa nafasi ya kutetewa/kupewa nafasi ya kuwakilishwa kisheria).


Sina nia ya kumtetea au kuonesha kua Wema Sepetu hana kosa kwa utumbo aliofanya, au Amber Rutty kwa upuuzi aliofanya. Hapana, nia yangu vyombo husika vifate sheria stahiki ili hukumu zao ziwe na nguvu (hata mbele ya mahakama wakiamua kukata rufaa ya hizo hukumu).
 
Atanyooka maana ndio aina ya maisha aliyoyachagua
 
Kuchqmba kwingi... Ameishia pabaya sana
Aendelee kuuza uch na kuuza mashoga bangi imemmaliza
 
Unajua kusoma na kuelewa ulichosoma? Kama jibu ni ndiyo basi nakushauri usome tena habari, pengine kuna sehemu umeruka.
 
Jamani hebu tuwe serious kidogo.
Yani miaka 2 tu ndio nini sasa.
Huyu ilitakiwa mpaka awamu ya 6 asote tu.
Hiyo ni adhabu ndogo sana
 
Tunakoelekea.....utasikia mjumbe wa mtaa anaoishi Wema Sepetu kamfungia kuonekana mtaani kwake kwa muda wa miaka miwili kutokana na video yake iliyosambaa mitandaoni ambayo haiendani na maadili ya Watanzania.🤗🤗🤗🤗
 
Unajua kusoma na kuelewa ulichosoma? Kama jibu ni ndiyo basi nakushauri usome tena habari, pengine kuna sehemu umeruka.
Wewe kweli macho mdiliko kama jina lako linavyosema,

Nimesoma vizuri na kuelewa vizuri, na ndio maana nikatoa ushauri/mtazamo wangu kwa hicho chama, ili hata kama chama kikimpa adhabu Wema basi iwe kisheria, na asiwe na uwezo wa kukata rufaa mahakamani na mahakama kuweza kutengua hukumu kwa kigezo wametoa hukumu bila ya kufata sheria....

Kwanza tambua kitendo cha chama kuomba mamlaka husika kukataa kupokea utetezi wake ni kosa kisheria, tena ni kosa ambalo linapingana na katiba ya nchi. Hakuna mtu/mamlaka ambayo inauwezo wa kukataa ushahidi wa mshtakiwa. Inapaswa ipokeee na itolee maelezo sababu ya kukataa kuutumia katika hukumu itakayo toa (yani mfano wangesema "tumepokea utetezi kuwa Wema alivyokataa kuitikia wito wa kuja kwenye baraza la chama kusikiliza mashtaka yake alisema hakuwa nchini, ila ushahidi unaonesha alikuwepo nchini na amedharau makusudi, hivyo tunakataa utetezi huo).

NB Hio kauli tu inauwezo wa kumsababishia Wema akakata rufaa mahakamani, na mahakama ikatengua adhabu zote alizopewa.

Pili, hata kama chama kilifanya juhudi za kumtafuta na kushindwa kumpata, wanapaswa kutumia kigezo hicho wakimpata ajitetee kwanini hakuitikia wito kwanza, halafu ajitetee kwanini amesambaza video ambayo anajua ni kinyume na sheria za nchi. Halafu ndio watoe hukumu.

Tatu, mimi natamani afungiwe hata maisha asijishughulishe na maswala ya filamu kwasababu amejisahau kua yeye ni kioo cha jamii, na anapaswa kua mfano mzuri kwa mashabiki pamoja na chama cha filamu nchini. Na si kua mfano mbaya kwa mashabiki zake pamoja na chama cha filamu.

Nne, usipende kuropoka mambo ambayo akili yako haina uwezo wa kuchanganua/kuelewa na wala si size ya upeo wako wa kiakili. Uliza kistaarabu uelimishwe
 
Duuh miaka miwili amepigwa pin kwenye filam sasa si watamuua na njaa jamani dada wawatu
 
Jamani hebu tuwe serious kidogo.
Yani miaka 2 tu ndio nini sasa.
Huyu ilitakiwa mpaka awamu ya 6 asote tu.
Hiyo ni adhabu ndogo sana
Avatar yako umeweka picha ya Quran kama sikosei
 
CHama cha wasanii nacho wamfungie pia,TAFU nao wamfungie,TCRA wamfungie,TBS,TANROAD,TFDA na ikiwezakana hata TRA wamfungie kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…