Baada ya Bodi ya Filamu kumfungia Wema Sepetu, Chama cha Waigizaji Kinondoni nacho chamfungia

Umeandika mengi lakini sijaona point yako:
1. Chama kinasema kilimtumie wito akadanganya yupo nje ya nchi. Kama alidharau unataka wampigie magoti? Kwanini hakwenda kujitetea kama ana huo utetezi?
2. Chama kimesema utetezi aliotoa usikubalike kwani hauna mashiko. ie. anasema ni utoto ulimponza na hatarudia tena wakati alishaonywa siku za nyuma na tena ni serial offender aliyepatikana na hatia ya kumiliki msokoto wa bangi!
Ule wakati wa kubembelezana ulishapita na upepo wa Kikwete. Omba Mungu wakati urudi nyuma na hoja yako itakuwa na kazi.
 
Watu kama nyinyi mngepewa mamlaka nchini, basi mngekua mnafunga jela mpaka panya, paka, nzi na mbu.

Hivyo vyote vinavyosemwa katika mitandao, press conference na kuandikwa katika magazeti havina mashiko katika kikao cha nidhamu kwa taarifa yako.

Vitu vitakavyo jadiliwa katika kikao hicho ndio vitabakia kua ushahidi. Na kikao cha nidhamu hua kina hatua zake za kufuatwa;

1) Hatua ya kwanza ni Ufunguzi wa kikao cha nidhamu na mwenye kiti.
2) Hapa mshtakiwa anasomewa malalamiko dhidi yake na mwenye kiti.
3) Mlalamikaji anatoa hoja zake dhidi ya mshtakiwa, akiambatanisha video yenyewe alioiposti yenye maudhui mabaya. Pia anatoa hoja zake za malalamiko dhidi ya mshtakiwa ya kua walimuita na alikaidi amri au alidharau kwa makusudi (pia wanatoa ushahidi juu ya wito waliompa na uongo aliotumia kua hayupo nchini).
4) Mwenye kiti anafunga hoja za mshati na kisha kufungua mlango wa nafasi ya mshtakiwa kutoa hoja zake za utetezi wake dhidi ya kosa alilofanya na na utetezi wa kosa la kudharau wito wa kikao.
5) Mwenye kiti ana ahirisha kikao na kutaja muda au siku ta kutoa hukumu ya kikao baada ya kuangalia ushahidi wote na utetezi uliofanywa.

Usifikiri vikao vya nidhamu na hukumu zake zinatoka kama unavyofikiria wewe, kuna sheria za kufuatwa. Sio zinatoka kama magazeti ya udaku au ticketi za daladala.

Umeshazoea kuona viongozi wanavyokurupuka tu kufanya maamuzi yao basi unahisi hakuna sheria za kufuatwa, mtu akiwa na mamlaka basi ana haki ya kukurupuka na kutoa hukumu yoyote anaayohisi sawa???

Mtu hata kama amefanya mauaji, ana haki zake za kisheria na za kimsingi, na niwajibu apewe hizo haki zake zote, na kuna hatua za kufuatwa ili mpaka ahukumiwe. Bila hivyo basi kusingekua na mahakama wala rufaa katika kesi.

#kama hujaelewa usinikere, hebu niache
 
Mwenyewe keshaita na ''waandishi wa habari'' kakiri kosa na kusema ni ''utoto'' ulimponza wewe unataka kurudi kinyume nyume kama Amber kinyesi! Vipi mazee!
 
Mwenyewe keshaita na ''waandishi wa habari'' kakiri kosa na kusema ni ''utoto'' ulimponza wewe unataka kurudi kinyume nyume kama Amber kinyesi! Vipi mazee!
Sista fei naona hauelewi tu ukiambiwa swala la kuita press conference halina tija katika kikao cha nidhamu na adhabu yake.

Ila nahisi wewe akili zako zipo chini, umezikalia, badala ya kua kichwani. Nawaonea huruma sana walimu waliokufundisha shule.
 
Hivi mbona diamond hawakumpa adhabu yoyote kali na alikua anapost ya ajabu zaid ya wema.
Kukiss na mpenzi wako na kupost ni kosa gani mbona watu wanataka kuturudisha enzi za mawe na mtu kaomba radhi hadharani kwanini wanayakuza??

Serikali nayo inatafuta kufunika upuuzi wao wanaofanya kupitia wema sepetu. Kuna mambo makubwa ya kuongelea kama nchi lakini sio kila siku wema sepetu. Na wanajua watanzania tunavyopenda udaku lazima upepo uhamishwe na wema sepetu. Too much aaaaagh
 
Sista fei naona hauelewi tu ukiambiwa swala la kuita press conference halina tija katika kikao cha nidhamu na adhabu yake.

Ila nahisi wewe akili zako zipo chini, umezikalia, badala ya kua kichwani. Nawaonea huruma sana walimu waliokufundisha shule.
Lina uhusiano. Amekiri na hakutaka kuitikia wito. Ina maana amekubali wafikie uamuzi bila yeye kuwepo. Unajua walau sheria za vikao vya nidhamu? Ukikaidi wito hubembelezwi na kikao kinaendelea na kutoa adhamu kulingana na ushahidi uliopo mezani! Kama akili zangu zipo chini lakini zinafanya kazi ni vizuri zaidi kuliko zako zilizopo juu lakini haziwezi kuona mantiki ya hili suala.
 
Kama ulikua hujasoma sheria ya makosa ya mitandao kutuma picha au video chafu, hii sheria mpya, Wema Sepetu anaweza akatumikia kifungo cha Miaka7 jela au kulipa fine ya sh millioni 20.

Sasa hizo hukumu za chama ni cha mtoto. Wala sio za kupigia kelele.
 
What is your point? Mahakama na vyama ni entities mbili tofauti kabisa.
 
Kuchqmba kwingi... Ameishia pabaya sana
Aendelee kuuza uch na kuuza mashoga bangi imemmaliza
mashoga anawataka Makonda sasa atauza wa wapi maskini mtoto huyu, yaani kapigwa kote bora aolewe ukoooo aendeleze libeneke la kuliwa kiboga na huyu bwana mende future husbandee
 
Najiuliza tu, Kwa mfano baada ya mwaka mmoja BASATA wakimruhusu Wema kuigiza, tamko la chama cha waigizaji wa wilaya Kinondoni litakuwa bado lina mashiko? Kuna sababu gani wao kufungia baada ya mamlaka ya juu kuliko wao kufanya hivyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…