Baada ya Chama kugaragazwa Kura za Mchezaji Bora wa Wiki, ipi nafasi ya Simba Robo Fainali CAF?

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Mchezaji maachachari wa Al Ahly Mahmod Kahraba amemgaragaza Chama katika kuwania nafasi ya Uchezaji bora ya wiki. Ambapo Raia wa misri ambao wanashabikia timu hiyo walipiga kura na kumuwezesha kuibuka kinara.

Simba SC atamaliza nafasi ya pili kwenye kundi lake. Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni ni lazima apangiwe kucheza na washindi wa makundi mengine.

Washindi wa makundi mengine ambao wana uhakika wa kumaliza juu ya msimamo ni pamoja na;

1. Mamelodi Sundown

2. Wydad Casablanca

3. Esperance De Tunis

Hivi ni Vigogo au Miamba ya kiafrika ambapo sote tunafahamu kuwa USHINDI kwao ni lazima. Iwe jua au iwe mvua.

Kwa upande wa Simba, inafahamika kuwa hawapo katika ubora wao ambao unafanana na ule wa akina Miqquisone. Hata kufuzu kwao ni kwa sababu walipata fursa ya kuwekwa katika kundi jepesi lenye timu dhaifu kama Horoya AC na Vipers SC.

Ipi nafasi ya washiriki hawa wenye matumaini ya kufika nusu fainali na wakijua kabisa team yao sio ya ushindani kama walivyo wenzao Yanga SC?

 
Huu ni wehu.. si ni ww ndo ulikua unasema haya mambo hayana maana?

Sasa ni aje unalinganisha na nafasi kivipi?

Halafu mbona tayari Chama ameshakua mchezaji wa wiki,
ameshashinda goli la wiki?

Unahaha kama samaki mkizi..
 
Yaani tangu watambue wao ni ma Mbumbumbu wamekua waki komaa na vitu vidogo vidogo vya kipuuzi Kwa kuvitolea macho.

Tuzo za CAF za wiki hazina maana yoyote zaidi ya kuzifanya kurasa za CAF katika mitandao kuwa active.

Jamaa tangu timu Yao kukosa vikombe, wanajihusisha na vitu vidogo vidogo sana.
 
Huu ni wehu.. si ni ww ndo ulikua unasema haya mambo hayana maana?.sasa ni aje unalinganisha na nafasi kivipi? halafu mbona tayari Chama ameshakua mchezaji wa wiki..
ameshashinda goli la wiki?
Unahaha kama samaki mkizi..
Amekuwa player of the week kutokana na chanzo kipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…