Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 94
- 307
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Beda Nyaki amehitaji kupata muda wa masaa mawili kuweza kutafakari kama ataendelea na kusoma uamuzi aliotakiwa kuusoma tarehe 23 Januari 2025 juu ya shauri la Dkt. Wilbroad Slaa au lah.
Hakimu Nyaki ameomba kupata muda huo wa kutafakari kutokana na kuibuka kwa hoja mahakamani iliyoletwa na mawakili wa upande wa Jamhuri ya kuwa wamekata rufaa katika Mahakama ya Rufani juu ya uamuzi uliotewa jana Januari 30, 2025 katika mahakama kuu ya Tanzania.
Pia soma > Pre GE2025 - Dkt. Slaa ashindwa kufikishwa Mahakamani kutokana na changamoto za usafiri
Mawakili wa upande wa utetezi wamepinga hoja ya rufaa na kuieleza mahakama kuwa kukatwa kwa rufaa hakuizuii mahakama kutoa/kusoma uamuzi ambao ulikuwa upo tayari hivyo walimuomba Hakimu Nyaki kuweza kutoa uamuzi huo.
Katika hatua nyingine Wakili wa upande wa utetezi Peter Madeleka amemuomba Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira kuwapokea ili waweze kutumia njia ya maridhiano kuweza kumsaidia Dkt. Slaa katika mashauri yanayomhusu.
Tarehe 23 Januari 2025 mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilipanga kutoa uamuzi juu ya pingamizi la uhalali wa mashtaka aliyofunguliwa Dkt. Slaa hata hivyo haikuwezekana kwa sababu upande wa utetezi ulifungua shauri katika mahakama kuu ya Tanzania kuomba mapitio juu ya mwenendo wa shauri hilo mpaka maamuzi yalipotoka jana.
Kwa upande wake Wakili Paul Kisabo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania(THRDC) amesema mtandao huo unalaani mwenendo wa kesi nzima ya Dkt. Slaa huku wakisema kuwa hajatendewa haki.