Baada ya Diamond Platnumz kutangaza kuhamia rasmi Yanga SC nami nina huu Ujumbe muhimu kwake

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
"Kupitia Birthday Party yake hii Rafiki yangu mkubwa Haji Manara na Mimi Diamond Platnumz leo natangaza rasmi Kuhamia Yanga SC kwa Kuishabikia kwani Kwangu Mimi alipo Manara na Mimi nipo huko huko"

Chanzo: Mitandao mbalimbali

Haya Diamond Platnumz nami GENTAMYCINE nakuambia kuwa kwa Madeni makubwa uliyonayo huku TRA nao wakitaka Kodi yao ilikuwa ni lazima Ujipendekeze Kwao.

Diamond Platnumz wenye Akili Kubwa na Nyingi akina GENTAMYCINE tunajua umelazimika Kujipendekeza kuhamia huko Yanga SC kama Sharti Kuu ulilopewa na Mtunza Fedha Mkuu ( akiwa Waziri ) na Mstaafu Mmoja mwenye Ushawishi mkubwa Serikali hii ya Mama pamoja na Mwanae ( ambao Wote ni wana Yanga SC ) ili waweze Kukusaidia kwa Mama ili azungumze na wenye Kodi yao na Wasikukabe Koo ukaibika na Umasikini kukupigia Hodi na Ukaumbuka.

Kingine Diamond Platnumz tuna Taarifa kuwa Unaogopa sana jinsi Serikali ya sasa ( ya Mama ) ilivyo Jirani na Msanii Mshindani wako Harmonize ( Konde Boy ) na kumpa 'deals' nyingi za Matamasha ya Kiserikali hivyo umeamua kuja na huu Mkakati ili Wakubwa wengi wa Yanga SC na ambao wana Ushawishi mkubwa kwa Mama, Serikali yake na Chama Tawala cha CCM ili usisahaulike na Wewe uweze Kutumika na Kupendwa kama ulivyokuwa katika Serikali ( Utawala ) wa Hayati ( Baba ) aliyetuaga tarehe 17 Machi, 2021.

Tunajua Wewe ( Diamond Platnumz ) ni Kigeugeu / Mnafiki na Opportunist mkubwa kwani hata Kipindi cha Hayati ulijifanya ni mwana Simba SC kwakuwa ulijua Hayati nae alikuwa ni Mnyama ( Simba SC ) hivyo ungejionyesha ni mwana Yanga SC ingekuathiri kwa namna au nyingine kwa Fani yako, Biashara zako na mambo yako yale mengine uliyokuwa ukiyafanya na Mmoja wa Mtoto wa Mstaafu Mmoja Wewe ukiwa kama Begi lake au Punda wake wa Kutukuka.

Haya Sisi wana Simba SC ( GENTAMYCINE ) nikiwemo tunakutakia kila la Kheri huko Yanga SC unakohamia sasa ili kumfuata Rafiki yako Haji Manara ila tambua CCM ambayo pia una Uhusiano wa 85% na Yanga SC kwa mwaka 2025 Kipindi cha Kampeni itamtumia mno Msanii Mshindani wako Harmonize ( Konde Boy ) katika Kampeni zake zote na Wewe hauko kabisa katika Mipango yao kwani Mama alishakusoma Undumilakuwili ( Unafiki ) wako Kwake na kwa Watanzania tokea ukiwa Karibu / Jirani na Hayati Baba hivyo hakuna utakachokipata pamoja na huku ( huko ) Kujikomba Kwake ( Kwao )

Nisalimie sana Haji Manara sawa?
 
Diamond ni opportunist hata mwanzo hakua simba alijiweka tu upande huo kwa sababu za kimasilahi. Kwa kipindi hicho yanga ilikua ni timu ambayo haiwezi hata kujiendesha inatembeza bakuri la michango wakati wa mechi sasa diamond aungane nao kwa masilahi gani, hata kwenye maisha nyakati zako za shida ni ndugu na marafiki wachache sana ndo watakua karibu nawe.. sasa hivi diamond kaona upepo upo upande wa yanga nae kaelekea uko. Shabiki hawezi kuhama timu yake na diamond sio shabiki ni opportunist tu. Sioni kama kuna sababu yoyote ya kumuandama, mfanyabiashara yoyote lazima ajiweke kwenye nafasi ya kupiga pesa. Ila kiuhalisia diamond sio shabiki wa simba, yanga wala soka kwa ujumla. Hata kwa sasa anadai yeye ni mwanaccm siku chadema wakichukua nchi usishangae akaukana uccm wake anaojinadi nao sasa hivi.
 
Povu lote hili Kisa mtu kaamua kuhama timu..
 
Mdogo wangu/mwanangu GENTAMYCINE / GENTAMYCIME , kongole kwa hu uzi.

Sifa kubwa ya Watanzania ni UNAFIKI.
Alichofanya huyu Nassib ndicho ambacho wengi wetu tunafanya katika maisha yetu ya kila siku huku mitaani,sema ni kwa kuwa tu hatupo kwenye "umaarufu" na wala hamna kamera ndio maana tunajiona sisi hatuwezi kufanya alivyofanya Nassib.

N:B; Nimekufuatilia kwa kipindi kirefu na kugundua kuwa una kipaji kikubwa sana cha kuunga nukta (connecting dots) na kupata kitu ambacho kama sio halisi,basi kitakuwa kinakaribiana na uhalisia kwa zaidi ya asilimia sabini na tano (75%+).

Naomba nikushauri utumie kipaji hicho vyema katika kujipatia kipato maradufu na kujenga nchi kwa kulipa kodi na kusaidia jamii.

Wewe ni mtunzi/ mwandiahi mahiri sana wa hadithi ambazo zinakaribiana na ukweli kwa asilimia kubwa sana.

Mungu Baba wa Mbinguni akubariki sana.
 
Jamaa na nyimbo zake Kama kaanza kupoteza ushawishi hivi tofauti na miaka michache nyuma au sjui ni mimi nimeacha kumfatilia
Umaarufu wake umeshuka. Pamoja na muziki wake vile vile skendo na kuyaanika maisha yake hadharani ilisaidia kumpaisha(kumpa kiki) hii mbinu sasa hivi inatumiwa na wengi sana na sio wanamuziki tu hata wacheza mpira, wanasiasa n.k ndo maana unaona taratibu umaarufu wake unashuka kwa sababu upinzani wa kutafuta kiki umekua mkubwa. Mfano kwa kipindi hicho mahusiano yake na zuchu yangekua habari ya mjini kwa jinsi wanavyojianika hadharani ila sasa kuna couple nyingi zinazotaka kiki kama harmonize na kajala, ujakaa sawa itaibuka tetesi mobeto yupo na rick rose badae kidogo utasikia vunjabei anatoka na jokate ushindani wa kiki umekua mkubwa sana kiasi kwamba skendo za diamond sasa hivi hazihit kama zamani
 
Mwambie huyo chaijaba
 
Okay

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Mwamba unahaha sana..!! Upenzi wa timu ni hiari ya mtu..!! Kama vipi nawe hamia kwetu.
 
Tafadhali naitwa GENTAMYCINE na siyo huyo Tapeli na Aliyeiiga Brand ID yangu huyu GENTAMYCIME sawa Mkuu?

Asante kwa Ushauri wako Kuntu ambao nakuahidi Nitaufanyia Kazi kwa Maslahi ya Maisha na hata Maendeleo yangu.
 
Pumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…