Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka, je Benki zitapandisha riba za mikopo?

Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka, je Benki zitapandisha riba za mikopo?

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Watumishi wa umma watamkumbuka sana Magufuli kwenye mikopo.

Kabla Magufuli hajachukua nchi mwaka 2015 riba za mikopo ya kawaida ya watumishi ilikua ni kuanzia 20% hadi 25% kwenye mabenk yetu. Ilikua ukokopa milioni 10 kwa miaka 5 utalipa milioni 20.

Baada ya Magufuli kuingia alizishawishi bank kupunguza riba za mikopo ya watumishi na ya kibishara. Bank kubwa zinazotumiwa na sehemu kubwa ya Watanzania kama CRDB, NMB zilikubali kupunguza riba ya mikopo ya watumishi kutoka 22% hadi kati ya wastani wa 15%. Hii ni achievement kubwa.

Magufuli aliyashawishi mabenki pamoja na kuyalazimisha kutafta vyanzo vingine vya pesa kwa kuhamisha pesa zote za serikali kwenda benki kuu na pia kushusha riba ya dhamana za serikali jutoka 16% hadi kati ya 6%-9%.

Zamani mabenki ya kibiashara hayakua na shida sana na wateja wadogo wadogo kwa sababu yalikua na uhakika wa kuikopesha serikali kwa 16%. Baada ya Magufuli kushusha kiwango cha mikopo ya serikali angalau banks zikalazimika kutafuta wateja wadogo wadogo na kushusha riba ili kuvutia wakopaji wengi.

Bank za Tanzania zilizoea kufanya biashara na serikali ya Tanzania na sio kufanya biashara ya kukopesha wanachi ili kukuza uchumi na kuongeza mzunguko wa pesa kwenye uchumi. Banks zilikua na uhakika wa mkopaji mkubwa ambae ni serikali na anakopa pesa nyingi na analipa vizuri.

Sasa je, baada ya Magufuli kuondoka, banks zitaturudisha kule, maana hizi zilikua jitihada binafsi za Magufuli, je tutarudi kwenye riba 25%?.
 
Banki ipi ilipungiza riba wakati wa mwendazake.
 
Una Uhakika na Unachokiandika kweli? Wakati wa Mwendazake Benki zilipunguza riba ya Mikopo kweli? Ama ndio ziliongeza?
 
Back
Top Bottom