Baada ya DP World, tukumbuke kipande cha Loliondo

Baada ya DP World, tukumbuke kipande cha Loliondo

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,120
Reaction score
3,468
Nimetafakari sana haya nauzo ya ardhi za Tanganyika,

Hapo mwanzo kulikuwako Tanganyika ikatawaliwa na Julius K Nyerere akang'atuka akamrithisha Ally Hassan Mwinyi nchi ikiwa haina tobo wala kiraka. Ikawa jioni ikawa asubuhi Mwinyi akawa madarakani.

Mwinyi akatawala akiwa ni mtoa ruksa, tukawa ruksa kufanya chochote ili mradi tusivunje katiba ya nchi. Mwinyi katika kutembea tembea duniani akakutana na Mwarabu akamsimulia jinsi anavyoipenda Tanzania hasa Loliondo akakaribishwa, ikawa jioni ikawa asubuhi Loliondo ikamilikishwa kwa Mwarabu.

Asubuhi na mapema Mzee Mkapa aka chukua nchi kwa uwazi na ukweli tukaanza kuuza mali zetu za ndani tukauza hadi tukawashangaza waliozinunua mwisho wa siku tukaamza kuwa ombaomba tena, ikawa jioni ikawa asubuhi.

Kikwete akachukua nchi tukaahidiwa maisha bora tukaishi kwa matumaini ya ahadi ya kuku kuwanyonyesha wanawe bila mafanikio jua likazama asubuhi wakaibuka waokota makopo.

Asubuhi kumekucha tukaambiwa asiyefanya kazi na asile kabisa. Tukakaza mikanda kwa kazi tusizokuwa nazo miaka mitano ilikuwa ya moto tukaanza kuona majengo mbalimbali barabara madaraja ya kisasa, jua likawa limezama mapema

Jua likachomoza tukadhani kazi imekamilika tukaambiwa kazi iendelee, tumeendelea tukajikuta DP WORLD eti ni mwekezaji wa Bandari za Tanzania. Uwekezaji si tatizo kamwe tatizo liko katika vipengele hivyo tata ambavyo vikifanyiwa marekebisho siyo tatizo tena kwa wao kuwekeza.

TUKIMALIZA HILI LA DP WORLD TUCHIMBUE MKATABA WA PALE LOLIONDO NA TUJUZWE MKATABA HUO ULIJADILIWA NA BUNGE LIPI NA MASLAHI YA TAIFA NA MKATABA HUO NI YAPI. TUJUZWE NINI HATMA YA UWEKEZAJI HUO.

NINI SHUGHULI ZA MWEKEZAJI HUYO PALE LOLIONDO.
 
Uko sahihi kabisa maana walikuwa wanawahamisha wamasai eti kutunza mazingira kumbe kuna waarabu. Samia umetuuza tutakushitaki kwa Mungu
 
Bila Transparency tutaendelea na hizi ngonjera mpaka kingdom come.......

Hivi na ile Mikataba ya Gesi kuna anayejua ni nini kilichomo ?
 
Uko sahihi kabisa maana walikuwa wanawahamisha wamasai eti kutunza mazingira kumbe kuna waarabu. Samia umetuuza tutakushitaki kwa Mungu
Tanzania tunahitaji kuongozwa na mfalme wenye uchungu na nchi yake.
 
Watanzania tulipaswa kuwakataa wahuni mapema sana . Wahuni ni kama majambazi yanayotumia Bunduki. Ukiyachekea majambazi yanakuwahi na kukuua.

Wahuni Kwa Sasa hawana Cha kupoteza kiroho mana wamejikabidhi Kwa Shetani na mawakala wa kuzimu.
Hawa wanachoangalia ni madaraka yao na mianya ya Kupiga pesa na kuibia nchi muda wote.
 
Sio Loliondo tu tafuta na Mkataba wa Taniwati Njombe Nyerere aliowapa familia ya kifalme ya Uingereza

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Ndio kwanza leo nasikia km kuna ishu ya aina hiyo huko mjin njombe tena imefanywa na kubwa lao


Mwaga taarifa kuhusu hio ishu ya taniwati
 
Serikali ndiyo mzazi, ikiamua jambo liwe mtoto hana uwezo wa kupinga. Kipande cha loliondo ilitakiwa kipigiwe kelele kama za dp world tangu enzi zile za loliondo gate
 
Back
Top Bottom