Baada ya haji manara kuongea na uongozi wa simba unashida?

Ladder 49

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
7,918
Reaction score
20,037
Wakuu Habari zenu.

Haji manara ameondoka sawa ,ila tuwe wa Kweli Uongozi wa simba unashida mahali unafanya mambo mengi kiswahili sana.

Haji manara mwaka wa 6 yupo simba hajawahi kupewa mkataba sasa tafsiri yake ni kwamba hakuwa mwajiri wa simba ila walikuwa wanafanya mambo kiswahili wewe hamashisha mwisho wa mwezi uje uchukue laki 7 hapa.

Yaani hakuna hata mtu mwingine alieona huyo manara anatakiwa kupewa mkataba?
Timu inakuwa haina tathmini ya utendaji wa wafanyakazi wake .

Kwa namna haji manara alivyoongea yeye inaonesha alikuwa kama chawa wa mo,pakiwa na tatizo kwenye timu anapigiwa simu kwanza haji uko wapi njoo ofisini,yaani haji yuko karibu na tajiri wa timu na wakati yeye ni msemaji ambaye alikuwa kama anajitolea tu kwa cheo chake yuko mbali sana na bosi lakini yeye sasa yaani tajiri yuko karibu sana na msemaji wa timu kushinda wafanyakazi walioajiriwa na wasaidizi wake kwenye kazi ya timu ya simba.
Tajiri alitekwa haji alikuwa anataka aanzishe kelele haji hakawekwa ndani.kuwepo karibu na bosi hivyo kuna fanya bosi kutokueshimika na haji ndio maana anaongea kwa dharau na kuwaona wakawaida tu nyie, na wakati Ndio alitakiwa hawaeshimu , kama wafanyakazi wengine wanavyo kuwa kimya na wanaongea kwa adabu kwenye press za mo, wanaogopa mo ana hela.


Hiyo nafasi ya msemaji wa timu sijaona kama inahitaji mtu mwenye elimu kubwa kiivyo.ukiweka mtu msomi sana anawaza tu mshahara afanyi kwa kufia timu yeye ilimradi mpunga unasoma tu,mengine hayo mtajua nyinyi huko.

kikubwa kwenye timu ni watu wa tactics wakiwa vizuri viongozi na wachezaji wakiwa na furaha tu,hapo timu itacheza kwa kujituma na kila mtu ataipambania timu hapa sijaona umuhimu wa kuondolewa haji manara kwenye timu ya simba,kama na mshahara analipwa laki 7 kwa mwezi.

Simba Baada ya kupata mafanikio viongozi wamejisahau sana na wamelizika na kulewa mafanikio ndio maana Ukifika juu kinachofata ni kudondoka.
Kilichotokea sasa na hii ni kawaida kwenye watu wengi wakipata mafanikio lazima wagombane tu na hapo ndio inakuwa mwisho wao.


Wakikosa ubingwa msimu ujao watu hawata waelewa na Na wajiandae kukoga matusi kwenye mitandao ya kijamii. watu wataamini haji yuko sawa na viongozi ndio ni tatizo.


Nilikuwa nategemea Baada ya haji manara kuongea uongozi na wanasimba wote wangemuacha tu , Maana haji yeye alivyo ongea alikuwa anataka majibizano na simba maana anakuambia vingine kaweka akiba atakuwa anaviachia taratibu.kwanza hakuwa mwajiri wa simba sasa mnaangaika nae wa nini.

Kufanikiwa kwenye timu kuna mambo mengi sana simba bado sana kuchukua ubingwa wa Africa, inaendeshwa kienyeji sana.hawaja fika kokote kimataifa wana anza kugombana kila mtu anajiona mkubwa kwenye timu.

Nilichokiona kwa haji manara ni kwamba anajiona yeye ni mkubwa kuliko simba,hata mkataba mpya waliokuwa wanataka kumpa haji mshahara ulikuwa mil3 kwa mwezi kwa mimi nilivyoona alivyokuwa anaongea na waandishi wa habari pale,haji angekataa hiyo hela kwa kusema hela ndogo yeye anathamani zaidi ya hiyo hela. Kama angekataa hapo angeonekana yeye ndio mwenye shida. Na ndio ingekuwa njia Nzuri ya kumuondoa kwenye timu.

Viongozi wa simba ifike mahali waeshimu pia kazi ya mtu na kuondoa dharau,kama huku kitaa mtu uko stand ya bus hapo hapo mtu anakusimamishia gari unapanda anachukua chake na wakati hata wewe unaweza kufanya hivyo mwenyewe lakini wewe hiyo haikuhusu panda gari sepa kazi za watu hizo.mbona anapata hela kirahisi usijadili anapata hela kirahisi.

Tajiri wa timu anaumia haji manara akiwaambia watu kwenye page yake ya instagram kunyweni maji ya azam badala ya maji ya biashara ya maji ya tajiri, na wakati huo haji manara haja ajiriwa kutangaza biashara za tajiri yeye ameajiwa (hana mkataba wowote) na simba .


Kinachoendelea kwenye mitandao sio kidhuri maana na wachezaji wanaona pia. Kama leo chama mwamba wa Lusaka anaomba msamaha kwa mo na wakati hayo mambo yeye hausiki kabisa nayo.kisa kumsema vizuri haji manara .

Mo alivyo kwenye simba hakuna utofauti na haji alivyo kuwa kwenye simba yaani yupo lakini aeleweki yaani kama haji manara alivyokuwa anajitolea anachukua chake.

Ni hayo tu wakuu.
 
Mo amezidisha ushabiki na kusahau kua yeye ni mwekezaji. Anafikiria kama mshabiki anachosahau kauli yake ina impact kubwa sana kuliko shabiki mwengine yeyote. Sijui nini kilimtuma kuingilia ile live stream ya Chama? Imemuexpose kwa kiasi kikubwa. Haji Manara kapata tuta dakika ya 89.
 
Bugatti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…