Baada ya joto kuua zaidi ya watu 500 Canada, Dubai yatengeneza mvua feki kukabiliana na joto

Hii tech wameitoa iran iran huwa wanatumia drone na rocket maalum kutengeneza mvua iran imefika mbali mpaka kufikia uwezo wa kuhamisha mawingu ya mvua
Techinolojia hii ipo mataifa mengi sema huwa hawaitumii sana ni ya kitambo mno mbona
 
Hawa waarabu si wangeita mababu zetu wa kiafrika jamani mbona hii kitu huwa inawezekana na ni easy kabisa
 
Mvua feki?hivi Dubai hawanaga ilani jamani?
 
Tempering with nature..., hii issue sio ngeni hata Lowassa alisuggest kitu kama hki ila in the end madhara huenda yakawa makubwa...

Let nature take its cause, joto linazidi sababu ya uharibufu wa mazingira na global warming na bado hali itakuwa mbaya, suluhisho sio shortcut bali kuacha kuharibu mazingira...

Kumbuka hayo maji kwenye mawingu ndio hayo yalikwenda huko katika cycle ya maji.., sasa kuyatungua tu bila kujali jinsi ya kuyatunza na kukata miti hovyo na kuharibu vyanzo vya maji..., haiitaji rocket science kujua kwamba soon or later kama hatutabadilika tutakuwa history...
 
Sumbawanga mnalala mno.... Wakati wenu wa kutoka ni huu.

Uzeni utaalamu huko
 
Wenzetu Wana uwezo wa kifedha. Hii inanikumbusha mbunge mmoja miaka ya nyuma alipendekeza bungeni kuwa hakuna haja kuwepo shida ya maji nchini,tuyageuze maji ya bahari kuwa maji ya kutumia.mbona Arabuni wamewezaa.
Mwingine alipendekeza tutumie mkaa kusugua meno,hamna haja ya Colgate,tutaokoa fedha.jamii yetu ijifunze Kuchagua watu weledi,sio Kila mtu anafaa
 
Kwanini wasipande miti inayovumilia ukame kama midodoma na kuimwagilia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…