Baada ya Kakoko na Bashiru, sasa ni zamu ya Dotto James

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,419
Wale 'untouchables' waliokuwa wanapigiwa kelele na watanzania hatimaye wameanza kushushwa mmoja baada ya mwingine.

Baada ya Kakoko na Bashiru kushushwa sasa inafata zamu ya Dotto kushushwa. Wapo wengi, muda ukifika wote watenguliwe nyadhifa zao ili kuondoa ile sintofahamu iliyokuwa imejengeka miongoni mwa Watanzania.
 
Huyo Doto James, Mama Samia hapaswi kumchekea hata kidogo...................

Anapaswa kumtumbua Mara moja huyo mpwa wa Hayati Magufuli, ambaye utendaji wake alikuwa akimtii Hayati Magufuli, badala ya kuwatumikia Umma wa watanzania
 
Kipindi cha Channel ten cha polepole kipo kinaendelea au??
 
Ataachwa sababu ya heshima ya mwendazake
 
Tahadhari kubwa inahitajika,huyu bwana anajua wapi Meko alipokuwa anatoa fedha za kununulia Channel Ten na zile alizokuwa anagawa barabarani wacha za kumlipa yule kandarasi maarufu aliyejenga uwanja wa Chatto
 
Next is Biswalo Mganga na Jaji Feleshi. Hawa watu wameumiza sana watu nchi hii. Mama Samia afanye yake tu mama yetu
 
Kama ni fisadi lazima uende shimoni
 
Hamna lolote utaona tu huyo doto atapewa uDED ama UDC
 
Huyo Doto James, Mama Samia hapaswi kumchekea hata kidogo...................

Anapaswa kumtumbua Mara moja huyo mpwa wa Hayati Magufuli, ambaye utendaji wake alikuwa akimtii Hayati Magufuli, badala ya kuwatumikia Umma wa watanzania

Sasa ni zama za Abdul na Mchengerwa Samia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…