wadau nafikiri tujifunze yanayoendelea kule sudan kwani ndugu zetu wa kule jumapili hii watapiga kura kuhusu sudan kusini kuwa nchi,natamani na sisi tujitenge kutoka tanzania bara ili nasi wazanzibar tuwe huru kutoka mikononi mwa wadanganyika
Unataka kujadili mustakbali wa Muungano upi Son of Peasant?
Zanzibar wana Katiba yao, wapi Katiba ya Tanganyika?
Zanzibar wana Bendera yao, wapi Bendera ya Tanganyika?
Zanzibar wana Wimbo wa Taifa, Wapi wimbo wa Taifa la Tanganyika?
Aaaah! Mtu wa pwani usituangushe bana "mwingiliano/muingiliano(interaction)" ni matusi? hayo hatuyatarajii toka kwa mtu wa pwani, neno hilo litatafsrika baada ya maneno mengine mbele i.e ....wa...., .....baina...., .....kati ya....; then ukikusudia kutokea huko-fahuwa!