Baada ya Kauli hii ya Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally kumhusu Chama je, Wanasimba wakiambiwa hawajui Kufikiri watakataa na watanuna?

Baada ya Kauli hii ya Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally kumhusu Chama je, Wanasimba wakiambiwa hawajui Kufikiri watakataa na watanuna?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
"Nimekuwa nikiulizwa sana hili Swali kama Chama kuanzia sasa atacheza Michuano hii ya Kimataifa naomba niseme Chama hatocheza Michuano hii ya Kimataifa" ameandika Ahmed Ally ( Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Simba SC ) katika Ukurasa wake wa Mtandao.

Sasa kama Viongozi wa Simba SC walilijua hilo huku wakijua kuwa bado wanashiriki Michuano ya Kimataifa kwanini tu wasingeachana na Chama ambaye ni kama wamemsajili aje kutuchezea tu Ligi Kuu na Nafasi yake Simba SC ingemtafuta Mchezaji mahiri wa Kutusaidia katika Michuano hii ya Kimataifa?

Kama tayari Chama alishaonyesha 'interest' ya kurejea Simba SC kwanini tu Klabu isingemuomba aendelee kubakia RS Berkane mpaka Msimu unaisha ndipo arejeshwe akiwa Huru kabisa hata Kucheza Michuano hii ya Kimataifa kuliko Kumleta kama alivyo sasa na kuonekana ni kama tu kaja Kucheza 'Ndondo Cup' Tanzania?

Yaani Presha ya Chama kutakiwa na Yanga SC ndiyo imewafanya Viongozi wa Simba SC wamsajili / wamrudishe Klabuni Chama ili kukwepa lawama za Mashabiki na kukubali kama hivi alivyokiri Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally kuwa hatocheza Michuano ya Kimataifa ila ya Ligi Kuu na ile ya ASFC ndiyo atacheza?

Halafu kwa Upuuzi ( Upopoma ) huu GENTAMYCINE nikiwasema Simba SC naonekana Mbaya, Mnafiki mpaka hata Kuhusishwa kuwa Mimi ni mwana Yanga SC? Hivi wana Simba SC mkiacha kabisa Unafiki na Mahaba Niue yenu kwa Simba SC kwa hili la Chama kurejea na Kucheza tu Michuano ya Ligi Kuu na ile ya ASFC labda na Mapinduzi Cup huku akiwa hatumiki / hatotumka katika Michuano ya Kimataifa kwa sasa kama alivyokiri Msemaji Wetu Ahmed Ally hapa imetumika Akili Kubwa au ni Uthibitisho rasmi kuwa Sisi ni Mapopoma na tunastahili Kudharauliwa na Wapinzani Wetu Yanga SC?

Nichukieni ila sitoacha Kuwaelimisheni.
 
Daah we jamaa acha Leo nikuvue nyota moja Kati ya zile nne sasa umebaki na nyota tatu.
Pia punguza kulaumu Sana mwamba ,mengine yakikuzidi uwezo potezea tu.
Pumbavu univue Nyota nilipojiunga rasmi hapa JamiiForums mwaka 2013 nilidsrma kuwa nahitaji Kuvalishwa Nyota nawe / nanyi?

Hebu nitokee hapa tafadhali huna Akili za Kujibizana nami kwa Hoja zangu ambazo huwa naziweka / nazileta hapa Jamvini sawa?
 
Kuna Jamaa alikuwa akipaza sautì kwa mwenzie kuwa "Nyani haoni..." kwa kweeli sikusikia hapo mwishoni kwenye "..." Nkumbushe Tafadhali
Katika Kumuelimisha Mpumbavu kuna suala la Kumpumzisha ( kumpa Break ) kama usemavyo hapa? Jibuni Hoja zangu basi angalau hata mara moja moja ili niwaone kama mna Akili ambazo hata hivyo najua hamna.
 
Timu ligi kuu ilikuwa inachechemea. Kombe la Azam hilo hapo na ni muhimu.
Simba ingesubiri msimu iishe vipi kama angezoea mazingira na kupata form kule Berkane. Wangemuachia?
 
Timu ligi kuu ilikuwa inachechemea. Kombe la Azam hilo hapo na ni muhimu.
Simba ingesubiri msimu iishe vipi kama angezoea mazingira na kupata form kule Berkane. Wangemuachia?
Kwahiyo Kwako Wewe Chama alisajiliwa na Simba SC aje atusaidie Kimataifa hasa au katika NBC Premier League na ASFC? Nikiwaita Mapopoma ( Majuha ) mnakasirika wakati kumbe huwa nakuwa nipo sahihi 100% kabisa.
 
Mkuu lala..inatosha basi. Mtoto lala
Daah..unalaumu sana
Waambie wale Walionidhihaki, Walionishambulia mpaka hata Kunitusi hapa JamiiForums tokea ile Juzi niliposema ( katika Uzi wangu ) kuwa Simba SC haitotoboa mbele ya Orlando Pirates au Al Ahly Tripoli au TP Mazembe na kwamba hapa Robo Fainali tulipofika ndiyo mwisho waniombe Radhi vinginevyo wana Simba SC wote hapa JamiiForums mtanichukia na hamtoamini sawa?

Najua mengi ya Simba SC nitayamwaga.
 
1) chama akiendelea kukaa kule anawezapata form mwisho wa msimu asipatikane. Atatamuka full msimu ukianza

2) Ligi kuu pia ni muhimu,timu ilikuwa inayumba

3) kombe la Azam ni Muhimu.

Simba isingefanya vizuri kimataifa,ikaukosa ubingwa ligi kuu,ikaukosa Azam . Ikawa ya pili ligi kuu maana yake mwakani isingeshiriki kimataifa. Nafasi zingekuwa 2 Tz badala ya 4.
Ikaona Chama aje mapema kupambania Azam Federation cup.

Ukinijibu jibu kwa kila kipengele
 
Acha utoto mtu mzima unaoneka taahira.
Umezoea kusema uongo uongo na uzushi mwingi kila siku.Huaminiki tena endelea na kazi yako ya utapeli
Waambie wale Walionidhihaki, Walionishambulia mpaka hata Kunitusi hapa JamiiForums tokea ile Juzi niliposema ( katika Uzi wangu ) kuwa Simba SC haitotoboa mbele ya Orlando Pirates au Al Ahly Tripoli au TP Mazembe na kwamba hapa Robo Fainali tulipofika ndiyo mwisho waniombe Radhi vinginevyo wana Simba SC wote hapa JamiiForums mtanichukia na hamtoamini sawa?

Najua mengi ya Simba SC nitayamwaga.
 
Daah we jamaa acha Leo nikuvue nyota moja Kati ya zile nne sasa umebaki na nyota tatu.
Pia punguza kulaumu Sana mwamba ,mengine yakikuzidi uwezo potezea tu.
Kwahiyo unamvua nyota kwasababu ametoa hoja ambazo huzipendi?
 
We jamaa kama itakuwa sio muandishi wa mwana sports basi utakuwa wa dimba sio kwa nyuzi hizi .
 
Back
Top Bottom