Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Wakuu,
Pongezi sana JamiiForums kwa kutupazia sauti mpaka maji yameanza kutoka na presha ipo vizuri tofauti na siku tatu za nyuma kabla ya maji kukata kukabisa.
Nimeona Waziri amekuja kujibu na kusema kati ya sehemu kuna huduma ya uhakika ya maji ni Mbezi Beach! Huu ni uongo mkubwa Wizara ya Maji, unaweza kuangalia mnyuzi za malalamiko nimeweka hapa ni hii ni mtu mmoja tu!
Huduma inazidi kuzorota kadri siku zinavyoenda, mpaka tunaanza kuamini huenda kuna watu wanafanya hujuma huku. Kila mwezi maji lazima yakate, bila taarifa yoyote, ukipiga simu kuuliza hupewi maelezo ya kutosha, ni mpaka msumbuane wee na ulete uzi JF ndio huduma inarejea.
Kwakweli inakwaza kuja kulalamika kila wakati kwa huduma ambayo siyo kwamba tunapewa bure, tunalipia na usipolipa bili unaondolewa huduma fasta.
Waziri Aweso Wizara ya Ardhi tunam vijana wako field wafanye savei kutoka kwa wananchi katika maendeoe mbalimbali ikiwemo Mbezi Beach, utapata uhalisia wa mambo kama huduma zinalidhisha kweli au lah. Hapa ndio utaelewa una mizingo mingi tu huko inakula mishahara bure, unless na wewe uwe sehemu ya hujuma hii tunayofanyiwa wananchi.
Baada ya kusema hayo, kuna baadhi ya mitaa kwa Zena hapa hapa maji bado hayatoki, muwaangalie na huko. Kukaa siku tu bila maji ni mateso, sasa fikiria siku 4 na hilo joto, mnatubanika bila kupenda, ni mateso bila chuki. Nakupongeza Waziri Wizara ya Maji kwa kuaddress hili taarifa ilivyoufikia ila kiukweli huduma bado hairidhishi.
Pia soma:
- Waziri Aweso: Tatizo la Maji Mbezi Beach Mkoani Dar Es Salaam limeisha. Kulitokea Hitilafu
- KERO - √ - Siku ya 4 Mbezi Beach hatuna maji, mpaka sasa hatupewi majibu ya kuridhisha hali inazidi kuwa tete. Si mje mng'oe na hizi mita zenu tujue moja