Baada ya kiapo mahakamani wananchi tukigundua shahidi kadanganya taarifa zake ipi nafasi yetu?

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Naomba kufahsmishwa na wajuvi wa sheria nafasi ya mwananchi anayegundua kuwa shahidi aliyeapa mahakamani amedanganya taarifa zake binafsi, taarifa husika ni jina kamili, umri, kabila na elimu.
 
Hivi kuna adhabu yeyote kwa mtu anaedanganya Mahakama? Hatua gani inachukuliwa dhidi ya mtu ambae amesema uongo baada ya kuapa? Kuna mfano wowote wa mtu aliyewahi kuadhibiwa kwa kudanganya Mahakama?

Amandla...
 
Kwa mfano mtu anasema alimaliza chuo mwaka flani na ukiangalia unaona alimaliza hio degree akiwa na miaka 18 tu.

#Airtel money-kutuma na kupokea pesa Ni buuuuuuure kabisa.
 
Hapo inategemea huyo aliyechukua kiapo yupo upande gani. Kama yuko upande wa Serikali, hakuna tatizo ila kama yuko upande mwingine linakuwa ni kosa kubwa sana na linaweza kuwa la ugaidi
 
Naomba kufahsmishwa na wajuvi wa sheria nafasi ya mwananchi anayegundua kuwa shahidi aliyeapa mahakamani amedanganya taarifa zake binafsi, taarifa husika ni jina kamili, umri, kabila na elimu.
Hili ni kosa la jinai linaloitea "perjury". Kwenye nchi zenye uhuru wa mahakama na mahakama zinaheshimika sawa sawa unaweza kupata kifungo gerezani cha kati ya mwaka mmoja hadi miaka mitano.
 
Mimi naona wakati umefika kwa viapo viondolewe serikalini, inaonesha watawala weusi wamerithi tu toka kwa watawala weupe.
 
Naomba kufahsmishwa na wajuvi wa sheria nafasi ya mwananchi anayegundua kuwa shahidi aliyeapa mahakamani amedanganya taarifa zake binafsi, taarifa husika ni jina kamili, umri, kabila na elimu.
Unapaswa kutoa taarifa kituo cha polisi, kusema uongo mahakamani ni kosa la jinai liitwalo "perjury"
 
Kale kamwanasheria ka airtel kalidanganya umri
 
Unapaswa kutoa taarifa kituo cha polisi, kusema uongo mahakamani ni kosa la jinai liitwalo "perjury"
Kosa la kuidanganya Mahakama lonapofanywa mbele ya hakimu au Jaji linaadhibiwa hapo hapo. Mfano ukipiga kelele Mahakamani. Hii inaitwa summary procedure.
 
Tofautisha perjury na contempt of court.Tena hata contempt of court kuna kesi zinaelekeza utaratibu ikiwa ni pamoja kuanda mashtaka na kusomewa kosa husika.
 
Naiomba hiyo kesi Mkuu.
 
Back
Top Bottom