Baada ya kipigo cha goli 8-2 kutoka kwa Bayern Munich, Barcelona imemtangaza Ronald Koeman kuwa kocha mpya

Baada ya kipigo cha goli 8-2 kutoka kwa Bayern Munich, Barcelona imemtangaza Ronald Koeman kuwa kocha mpya

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Ronald Koeman (57) ametangazwa kuwa Kocha mpya wa Klabu ya Barcelona ya Uhspania, akipewa mkataba wa miaka miwili na kulazimika kuacha kazi yake ya kuifundisha timu ya Taifa ya Uholanzi

7944BE85-0F15-494C-9E9A-A45C54381358.jpeg

Koeman ambaye ni raia wa Uholanzi anachukua nafasi ya Kocha Quique Setien, aliyefukuzwa baada ya Barcelona kupata kipigo cha aibu kutoka kwa Bayern Muchin cha goli 8-2

Koeman, ameichezea Klabu hiyo kutoka eneo la Catalonia kwa miaka 6 akiwa mmoja wa watu waliokuwa katika timu iliyoongozwa na Johan Cruff, maarufu 'Dream Team'

Alifanikiwa kushinda mataji manne ya La Liga na anakumbukwa kwa goli lake lililofanya Barcelona kushinda taji la Ulaya mwaka 1992. Koeman alikuwa chaguo la kwanza la Rais Josep Maria Bartomeu kuinoa Barca

Aidha, kuhusu Messi kutaka kuondoka Bartomeu amesema, "Nimeongea na Koeman na amesema nguzo ya tunachotaka kukijenga Barcelona ni Messi"
 
Timu imejaa mamluki kutoka Real Madrid, kuanzia uwanjani mpaka kwenye board kwahiyo Koeman bora afunge mabegi kabisa maana safari imewadia kabla hajaanza kazi 😂😂😂
 
Back
Top Bottom