Baada ya 'Korona' unadhani amsha-amsha itakayofuatia ni ipi?

funluverx

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2014
Posts
480
Reaction score
343
Nimegundua mwaka ni mdogo sana katika maisha,

Kama yalivyo mafupi maisha yenyewe. Hatahivyo vinaunogosha na kuukimbiza mwaka ni pamoja na MATUKIO (mnapigwa matukio, mnapigwa matukio, mkija kujistukia mwaka huo umeisha unakuja mwingine)

Ingawa mengine yanatokea tu kwa matakwa ya 'muweza' yapo mengine yanatengenezwa (Inaaminika)

Kubwa tuliloingia nalo mwaka huu ni hili la Vifo vinavyotokana na kadhia Iliyobatizwa jina la 'changamoto ya kupumua'.
Kwa uweza wa Jalali yote yatapita na maisha yataendelea.

Binafsi naamini hatahivyo, bila ya matukio basi maisha hayanogi.

Amsha amsha ya majadiliano, mivutano na marumbano ya hoja vyote kwa pamoja wakati mwingine hunogesha na kuleta ladha ya maisha.

Sasa tuwe watabiri kidogo;

Unadhani tunaweza kupigwa na sarakasi gani mara tu baada ya 'Korona' kuwa Historia?

Je, Pesa itakuwa nyingi mtaani tumwage sifa juhudi?? je, Kuna Wa/Mzito kufutwa Kazi ghafla?

Binafsi, naona siku si nyingi Pesa itakuwa bwerere mtaani kwa anaeitafuta kweli, pesa inaweza kuchapishwa mpya (kubadilishwa) muda si mrefu pia.

Nini utabiri wako wewe?
 
Bado sijapata maono yoyote ila kea paremeters zilizopo inaonesha
1.watoto watakuwa na akili Sana kuliko kawaida
2.mambo yanayotisha Kama vile bangi yanakwenda kuwa ya kawaida Sana hivi karibuni
3.watu itakuwa hawakutani Sana mfano ndugu ule umoja utapungua
 
Nachokiamini.mimi sasa acha kabisa siku zinakuja tutakua masikini wa kupitiliza kutakua hakuna pesa kodi zitakua zimebana kama vile tatizo la upumuaji. Watu watafunga mabiashara na kuishia kutanga tanga mitaani . Wasomi watafurika mitaani jobless kikubwa ni kumuomba Mungu maisha yabadilike haraka na viongozi wetu waangalie hatima ya miaka ya mbeleni. Asee tufanye kazi pia tungalie miaka mi3 mbele laa sivyo tutajikuta tuko katika hali mbaya sana ya kifeza . [emoji2962] 2021 TUTAFUTE PESA ZA KUFUKIA MAGEPU YA 2024,2025[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tusiochanjwa tutatengwa kama kisiwa, ila bado tutakomaa hivyo hivyo, hamna kuchanjwa. We chanjo gani mtu hadi mnahongwa pesa ili mchomwe?
 
Ninaamini Yesu yu karibu kuja kuwanyakua wateule wake, hautofika mwaka 2042, kwa mujibu wa unabii ulioko kwenye maandiko matakatifu.

JESUS IS LORD
Mwaka 2000 tuliambiwa hivyohivyo lakini😎
 
Nachokiamini.mimi sasa acha kabisa siku zinakuja tutakua masikini wa kupitiliza kutakua hakuna pesa kodi zitakua zimebana kama vile tatizo la upumuaji. Watu watafunga mabiashara na kuishia kutanga tanga mitaani . Wasomi watafurika mitaani jobless kikubwa ni kumuomba Mungu maisha yabadilike haraka na viongozi wetu waangalie hatima ya miaka ya mbeleni. Asee tufanye kazi pia tungalie miaka mi3 mbele laa sivyo tutajikuta tuko katika hali mbaya sana ya kifeza . [emoji2962] 2021 TUTAFUTE PESA ZA KUFUKIA MAGEPU YA 2024,2025[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Iwapo 2021 ndio unaopaswa uwe mwaka wa kufukia mageti sio ma-gap ya hiyo miaka ijayo basi twafa huko tuendako😳
 
Tusiochanjwa tutatengwa kama kisiwa, ila bado tutakomaa hivyo hivyo, hamna kuchanjwa. We chanjo gani mtu hadi mnahongwa pesa ili mchomwe?
Utajali kutoa kaufafanuzi mkuu?
Binafsi umeniacha pakubwa.
 
Nimegundua mwaka ni mdogo sana katika maisha,

Kama yalivyo mafupi maisha yenyewe. Hatahivyo vinaunogosha na kuukimbiza mwaka ni pamoja na MATUKIO (mnapigwa matukio, mnapigwa matukio, mkija kujistukia mwaka huo umeisha unakuja mwingine)

Ingawa mengine yanatokea tu kwa matakwa ya 'muweza' yapo mengine yanatengenezwa (Inaaminika)

Kubwa tuliloingia nalo mwaka huu ni hili la Vifo vinavyotokana na kadhia Iliyobatizwa jina la 'changamoto ya kupumua'.
Kwa uweza wa Jalali yote yatapita na maisha yataendelea.

Binafsi naamini hatahivyo, bila ya matukio basi maisha hayanogi.

Amsha amsha ya majadiliano, mivutano na marumbano ya hoja vyote kwa pamoja wakati mwingine hunogesha na kuleta ladha ya maisha.

Sasa tuwe watabiri kidogo;

Unadhani tunaweza kupigwa na sarakasi gani mara tu baada ya 'Korona' kuwa Historia?

Je, Pesa itakuwa nyingi mtaani tumwage sifa juhudi?? je, Kuna Wa/Mzito kufutwa Kazi ghafla?

Binafsi, naona siku si nyingi Pesa itakuwa bwerere mtaani kwa anaeitafuta kweli, pesa inaweza kuchapishwa mpya (kubadilishwa) muda si mrefu pia.

Nini utabiri wako wewe?
Ukomo wa muda wa Rais kubaki madarakani
 
Back
Top Bottom