Baada ya Kuacha Kazi Julius Nyerere Aliishi Nyumba Ipi Kabla ya Maduka Sita Magomeni?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
WAZEE WANA USEMI "CHINI KUNAKWENDA WATU"

Picha hizo mbili hapo chini hazihitaji maelezo mengi mengi ni picha za Abdul Sykes na Julius Nyerere na wake zao.

Picha ya Abdul Sykes imepigwa Government House katika Garden Party ya Gavana Edward Twining na mkewe Mrs. Twining miaka ya 1950 wakati akiwa kiongozi wa TAA.

Picha ya Nyerere imepigwa miaka ya mwanzo ya uhuru 1960s.

Wazalendo hawa wawili hakuna aliyefungua kinywa chake kueleza kuhusu urafiki wao wala kueleza historia ya kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Lakini kwa bahati historia za wazalendo hawa wawili zote zimeandikwa na kwa hakika ndiyo historia ya harakati ya kupambana na ukoloni wa Mwingereza kupitia chama cha TANU.

Wake zao Bi. Mwamvua na Maria Nyerere wameshuhudia yote kwa macho yao na wamesikia mengi kutoka kwa waume zao katika yale ambayo yalifanyika wakati ule.

Baada ya karibu miaka 20 kupita Bi. Mwamvua maarufu kwa jina la Mama Daisy alikutana na Mama Maria Ukumbi wa Diamond siku Mwalimu alipokuwa na mkutano wa kuwaaga Wazee wa Dar es Salaam mwaka wa 1984.

Mama Maria Nyerere alikutana na wanawake wa Dar es Salaam baada ya Mwalimu kumaliza hotuba yake ya kuaga.

Siku ile ndiyo kwa mara ya kwanza Mwalimu alimtaja Abdul Sykes hadharani.

Mama Maria alipomuona Mama Daisy katika kundi lile la akina mama, Maria Nyerere aliwaambia wale wanawake waliokutanika kumuaga, ''Huyu Mama Daisy na mumewe ndiyo waliotupokea mimi na mume wangu hapa Dar es Salaam.''

Maneno haya kanieleza Mama Daisy.

Ilikuwa miaka mingi imepita mashoga hawa wawili hawajaonana.

Prof. Shivji na jopo la waandishi wa historia ya Julius Nyerere, Prof. Saida Yahya-Othman na Dr. Ng'wanzi Kamata walipokuja nyumbani kwangu kunihoji kuhusu maisha ya Julius Nyerere alipofika Dar es Salaam niliwaomba wafanye juhudi wazungumze na Mama Maria kuhusu siku za mwanzo za TANU khasa ile mikutano iliyokuwa ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa Stanley na Mama Maria na Mama Daisy wakiwapo pale.

Sijui kilichotokea lakini kitabu kilipotoka imeelezwa kuwa Mwalimu aliishi nyumbani kwa Ally Sykes kwa miezi mitatu na imeelezwa kuwa chanzo cha taarifa ile ni Abbas Sykes.

Ukweli ni kuwa Mwalimu hakupata kuishi nyumbani kwa Ally Sykes na mkewe Bi. Zainab Mtaa wa Kipata bali aliishi na Abdul Sykes na mkewe Bi. Mwamvua Mtaa wa Stanley.

Kidogo nilisikitika kwani kwa kosa hili mengi yamewapita yaliyofanyika nyumbani kwa Mama Daisy.

Wakati ule hakuna aliyefikiria hata kwa mbali kuwa Julius Nyerere atakuja kuwa kiongozi mkubwa sana ulimwenguni na jina lake litafahamika kote duniani.

Laiti Mama Maria angezungumza...
1719660570020.png

1719660617998.png

1719660645755.png

1719660670709.png

Mbona hujaweka hizo picha?

Uzi mzuri japo lengo sijalielewa ni kutaka tu ijulikane Nyerere Dar alifikia kwa Sykes au ni nini naona kama hujaenda ndani zaidi au andiko halijafika mwisho mkuu
San...
Lengo ni hili.
Prof. Shivji at al wamenihoji na nikawaeleza historia ya Mwalimu na Abdul Sykes na nikashauri kuwa mengi atakuwanayo Mama Maria.

Hawakwenda kwa Mama Maria.

Kitabu kilipotoka yale niliyowaeleza hayakuwamo.

Soma para za mwisho uone kilichoandikwa.
 
WAZEE WANA USEMI "CHINI KUNAKWENDA WATU"

Picha hizo mbili hapo chini hazihitaji maelezo mengi mengi ni picha za Abdul Sykes na Julius Nyerere na wake zao.

Picha ya Abdul Sykes imepigwa Government House katika Garden Party ya Gavana Edward Twining na mkewe Mrs. Twining miaka ya 1950 wakati akiwa kiongozi wa TAA.

Picha ya Nyerere imepigwa miaka ya mwanzo ya uhuru 1960s.

Wazalendo hawa wawili hakuna aliyefungua kinywa chake kueleza kuhusu urafiki wao wala kueleza historia ya kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Lakini kwa bahati historia za wazalendo hawa wawili zote zimeandikwa na kwa hakika ndiyo historia ya harakati ya kupambana na ukoloni wa Mwingereza kupitia chama cha TANU.

Wake zao Bi. Mwamvua na Maria Nyerere wameshuhudia yote kwa macho yao na wamesikia mengi kutoka kwa waume zao katika yale ambayo yalifanyika wakati ule.

Baada ya karibu miaka 20 kupita Bi. Mwamvua maarufu kwa jina la Mama Daisy alikutana na Mama Maria Ukumbi wa Diamond siku Mwalimu alipokuwa na mkutano wa kuwaaga Wazee wa Dar es Salaam mwaka wa 1984.

Mama Maria Nyerere alikutana na wanawake wa Dar es Salaam baada ya Mwalimu kumaliza hotuba yake ya kuaga.

Siku ile ndiyo kwa mara ya kwanza Mwalimu alimtaja Abdul Sykes hadharani.

Mama Maria alipomuona Mama Daisy katika kundi lile la akina mama, Maria Nyerere aliwaambia wale wanawake waliokutanika kumuaga, ''Huyu Mama Daisy na mumewe ndiyo waliotupokea mimi na mume wangu hapa Dar es Salaam.''

Maneno haya kanieleza Mama Daisy.

Ilikuwa miaka mingi imepita mashoga hawa wawili hawajaonana.

Prof. Shivji na jopo la waandishi wa historia ya Julius Nyerere, Prof. Saida Yahya-Othman na Dr. Ng'wanzi Kamata walipokuja nyumbani kwangu kunihoji kuhusu maisha ya Julius Nyerere alipofika Dar es Salaam niliwaomba wafanye juhudi wazungumze na Mama Maria kuhusu siku za mwanzo za TANU khasa ile mikutano iliyokuwa ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa Stanley na Mama Maria na Mama Daisy wakiwapo pale.

Sijui kilichotokea lakini kitabu kilipotoka imeelezwa kuwa Mwalimu aliishi nyumbani kwa Ally Sykes kwa miezi mitatu na imeelezwa kuwa chanzo cha taarifa ile ni Abbas Sykes.

Ukweli ni kuwa Mwalimu hakupata kuishi nyumbani kwa Ally Sykes na mkewe Bi. Zainab Mtaa wa Kipata bali aliishi na Abdul Sykes na mkewe Bi. Mwamvua Mtaa wa Stanley.

Kidogo nilisikitika kwani kwa kosa hili mengi yamewapita yaliyofanyika nyumbani kwa Mama Daisy.

Wakati ule hakuna aliyefikiria hata kwa mbali kuwa Julius Nyerere atakuja kuwa kiongozi mkubwa sana ulimwenguni na jina lake litafahamika kote duniani.

Laiti Mama Maria angezungumza...
Mzee Mohamed Said Shukurani kwa kuweka historia kubwa hapa.

Nimepata kitabu cha Juma Volter Mwapachu "A Journey : My Life, Speeches and Writings".

Ndiyo naanza kukisoma sasa.

Kina historia kubwa inaonekana.

Umekipitia hiki?
 
"A JOURNEY" MY LIFE, SPEECHES & WRITINGS" KUTOKA KALAMU YA JUMA VOLTER MWAPACHU

Kuna wakati naamini hata William Shakespeare alikuwa anaishiwa na maneno kalamu ikabakia inaning'inia mkononi na wino kumkaukia.

Leo nimekitia kitabu mkononi.

Kwa hakika nimechelewa kukipata na sababu ni kuwa nilisubiri uzinduzi.

Kitabu kimetoka na mimi si mtu wa kukosa kuwa na kitabu anachoandika Juma Mwapachu kwani kawaida nakwenda kwenye uzinduzi na nakala yangu inapata saini yake.

Nilijihisi vibaya siku kaka Juma aliponiuliza kwenye simu kama nimekisoma kitabu chake kipya.

Hakika nilijisikia vibaya sana.

Juma Mwapachu ni mwalimu wangu na nimejifunza mengi kutoka kwake.

Nimepagawa.
Sijui nianze vipi.

Nianze kukieleza kitabu kina nini ndani au nianze kumueleza mwandishi?

Msomaji wangu naamini ushajua kuwa Juma Mwapachu ni mtu maalum kwangu.

Juma Mwapachu ni kaka yangu.

Sote tuliokuwa wadogo kwake hivi ndivyo tunavyomwita, ''kaka.''

Kwa wengine wadogo kwake ni kaka lakini kwangu mimi ni kaka na mwalimu wangu na nathubutu kusema ni ''Role Model,'' kwangu kwani tuko nilipofahamiananae mwaka wa 1967 wakati huo ndiyo mwanafunzi Chuo Kikuu yeye akiwa mmoja wa waliofukuzwa kwa tatizo la kugomea National Service.

Ulikuwa mwaka wa 1966 na nilijuana na Juma Mwapachu mwaka wa 1967 na nimekuwa mwanafunzi wake.

Nilikuwa na umri wa miaka 15.

Inatosha.

Nina picha nimepiga mwaka wa 1967 na kaka yangu Juma yumo.

Ilikuwa nyumbani kwa mama yetu, yeye dada kwake, Mary Mackeja, mama yake sasa Chief Edward Anthony Makwaia wa Siha.

Edward Makwaia amerithi kiti cha baba yake Chief David Kidaha Makwaia.

Mimi na Edward tumesoma darasa moja St. Joseph's Convent School.

Edward ambae tumezoea kumwita Ted ndiye aliyenijulisha kwa Juma Mwapachu.

Katika picha hiyo mdogo wake Juma Mwapachu, Wendo Mwapachu yumo.

Siku hii nilipokutana na Juma Mwapachu ilikuwa Birthday Party ya Ted.

Hawa wote niliowataja hapo juu wamo katika katika kitabu hiki kwa maandishi, picha na sura zao.

Kuna picha ni picha na kuna picha na sura za waliomo kwenye picha.

Baadhi ya hawa wametangulia mbele ya haki.

Si jambo la kawaida kuwa kitabu kimeandikwa na msomaji anasoma kitabu na kuyasoma maisha yake.

Msomaji anawajua waliotajwa na anajua waliyofanya.

Sasa nimepagawa kila ninapofungua kurasa.

Situlii kwenye kurasa wala kwenye sura moja.

Mshawawasha unanishika nataka kujua sura ya mbele kuna nini?

Kalamu ya Juma Mwapachu inaandika na kusema maneno pia.

Kitabu hiki ni safari kama jina lake linavyoonyesha na mimi nataka nisafiri behewa moja na mwandishi tena nimekaa pembeni yake.

Kitabu hiki kina mengi na kwa hakika ni kamusi tosha ya wanafunzi wa historia ya Tanzania kuwanacho katika maktaba zao kama kitabu muhimu cha rejea.

Nataka niwataje watu mashuhuri wachache ambao Juma Mwapachu kawaeleza kwa kina katika kitabu hiki: Dossa Aziz, Amon Nsekela, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Prof. Ali Al' Amin Mazrui, George Kahama, Dr. Reginald Mengi, Mark Bomani na kaka yake Harith Bakari Mwapachu.

Haya ni mepesi kwangu kuyaeleza lakini yapo mazito ya utawala bora, fedha na uchumi ambayo si mepesi kuyafahamu na kuyaeleza.

Napita kote humo kwa mwenda mkali.

Nimesoma course ya Kiingereza inaitwa, ''Reading Labaratory,'' mwalimu wangu alikuwa mama wa Kiingereza, Mrs. Grant yeye na mumewe Mr. Grant waliletwa Tanzania na British Council kuja kusomesha Kiingereza.

Katika course hii tulikuwa tunafundishwa kusoma kwa haraka bila kupoteza kile unachokisoma.

Hii ni silaha yangu ambayo imenisaidia sana katika maisha yangu ya uandishi.

Napita kuisoma hiyo miamba niliyoitaja hapo juu kwa kasi.

Baadhi ya miamba hii kama Dossa Aziz, Prof. Mazrui, Dr. Reginald, Mengi na Bakari Mwapachu tukijuana.

Kaka yangu Juma ndiye aliyenijulisha kwa Reginald Mengi tukafahamiana vizuri.

Naikumbuka siku hii kama jana.

Sikuwa najua kuwa Mengi na Juma Mwapachu walikuwa marafiki wakubwa.

Juma Mwapachu alinipeleka kwake ili nifanye tafsiri ya Kiswahili ya kitabu chake alichoandika: "I Can, I Must, I Will."

Mwalimu Nyerere hatukujuana lakini nimeandika historia yake kiasi nimeingia katika orodha ya watu watatu (Dr. Salim Ahmed Salim na Brig. General Hashim Mbita) mimi nikiwa wa tatu wao ambao wana taarifa nyingi za Mwalimu katika maktaba zao.

Hili waligundua waandishi wa Nyerere Biography, Prof. Shivji, Prof. Said Yahya Othman na Dr. Ng'waza Kamata wakati wakinihoji kuhusu historia ya Nyerere.

Kitabu kilipochapwa nikakuta hayo na yameandikwa katika kitabu hicho.

Sijipigii zumari.

Dossa Aziz nimemwandika sana pamoja na Mwalimu Nyerere kwani ni vigumu kuandika historia ya Nyerere ukamuacha Dossa Aziz.

Hawa walikuwa marafiki wakubwa kupita kiasi wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Juma Mwapachu alikuwa heshi kumtaja Dossa Aziz kila tulipozungumza historia ya uhuru wa Tanganyika.

Namsoma kaka yangu Juma Mwapachu na kitabu kinanigeukia mimi mwenyewe na kunisomesha ambayo sikuwa nayajua ya miamba hii ingawa mimi nilidhani sina jipya la kujifunza zaidi kuhusu wazalendo hawa.

Juma Mwapachu siku zote amekuwa mwalimu kwangu na kwa jamii ya wasomi wa Tanzania.

Ndani ya kitabu hiki kuna orodha ya vitabu na makala za kisomi alizoandika katika maisha yake.

Utachoka.

Kama nilivyotangulia kusema kitabu hiki ni kamusi ya historia ya Tanzania katika mabonde na milima iliyoteremka na kupanda.

Kitabu hiki ni kamusi ya kuwasoma baadhi ya watu mashuhuri Afrika ya Mashariki ambao Juma Mwapachu aliingiliananao akiwa mtumishi wa serikali na pia akiwa katika sekta ya biashara huria na wakati akiwa Balozi, na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Hiki ni kitabu kizito cha aina yake.
Kuna mengi msomaji atajifunza.

Kitabu hiki kimesheheni mambo mengi ambayo hawezi kuyapata kwengine kokote.

Juma Mwapachu amefungua mlango kwa wengine wanyanyue kalamu zao kuandika kumbukukumbu zao ili Tanzania iwe taifa ambalo wasomi na viongozi wake wanarejesha katika jamii uzoefu na mafunzo waliyopata wakati wakitumikia taifa hili.
 
Basi yule rafiki yako Ted mimi family kwa ndoa.

Nimefurahi sana kukipata hiki kitabu cha Mzee Juma Mwapachu na kujua umekifurahia.

Ukikimaliza na kupata wasaa nitafurahi ukikifanyia uzi maalum wa kukifanyia marejeo (book review) japo kwa dondoo.
 
Kiranga,
Nimefurahi kusikia hilo.
Fikra ya kukifanyia pitio ninayo.
 
Ushasimulia kila kitu na sasa unarudia yaleyale najua ipo siku utaandika mpaka kleist kumpa maji ya kunywa nyerere
 
Mnachi...
Kwani kuna ubaya gani kurudia jambo?

TBC wana kipindi ''Usia wa Baba,'' kinarushwa kila siku baada ya taarifa ya habari Mwalimu Nyerere anahutubia taifa miaka mingi baada ya yeye kuwa amefariki.

Kipindi hiki mimi nakipenda sana na naamini kina wasikilzaji wengi.

Sasa kama kuna mtu hapendi kusikiliza hotuba za Baba wa Taifa wala hakuna shida anabadili stesheni anaweka steshini nyingine.

Ikiwa wewe historia hii inakukera huipendi huna sababu ya kusoma au kusikiliza unapita wima au una-delete.
 
kaka mkubwa nchi Ina wahuni wengi wapya huyu mnachi ni mmoja wao wasikukatishe tamaa,timiza kusudi lako.

Back
Top Bottom