Baada ya kuangalia mechi kadhaa za Niyonzima akiwa Simba

Kwani Manara kaongea uongo?
Naam. Uongo uliokithiri. Kwanza hawajaweka kambi ya gharama Zanzibar, walifadhiliwa na Bkhresa kwenye eneo lake analojenga hoteli. Pili si kweli kwamba kikosi kimegharimu 1.3 billion kwa sababu hakukuwa na uwazi wowote wa gharama za usajili kwa mchezaji mmoja mmoja. Kama haisemwi (na Simba) wala haijulikani mchezaji gani kanunuliwa kwa kiasi gani, itajulikanaje kwamba usajili wote umegharimu kiasi fulani? Tatu ni kweli kwamba Simba imesajili majina makubwa kuliko timu zote msimu huu, lakini kuna tofauti kubwa baina ya majina makubwa na kikosi bora. Hiki ndiyo kikosi cha Simba chenye matokeo mabovu kuliko vyote kufikia raundi hii kwa miaka miwili iliyopita; kutoka kuongoza kwa pointi miaka ya nyuma hadi kuongoza kwa magoli msimu huu. Kusema kwamba hiki ndio kikosi bora ni uongo usio kifuniko. Si kweli kwamba Simba imekodi mwewe kuja Dar. Kwanza haikukodi ndege, imepanda ndege za kawaida zinazofanya safari za kawaida za Zanzibar-Dar. Na si mwewe, ni panzi, maana ndege inayobeba abiria chini ya ishirini haijatosha kuwa ni mwewe. Sasa ulitaka aseme uongo upi mwengine?
 
Simba hawakuwa na shida ya kusajili kiungo msimu huu! Walikuwa na viungo bora kabisa kama Mo Ibrahim, Mzamiru, Ndemla! Mkude, Majavi, Kotei n.k! Sijui kwanini waliamua kutumia hela nyingi kumsajili Haruna ambaye hana alichowazidi hao niliowataja!
Huko sahihi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…