Baada ya kubuni KKK, kalonzo aondolewa kutoka ulingo wa siasa

Baada ya kubuni KKK, kalonzo aondolewa kutoka ulingo wa siasa

Kabaridi

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2011
Posts
2,022
Reaction score
534
Vice president wa kenya alifanya hesabu zake vibaya kwa kuihama serikali teule ya jubilee na kuungana na cord. Sio kalonzo pekee ni wengi pia kwenye miungano mengine ambao wamelambishwa sakafu. Kwa kuungana na CORD alifikili kuwa wamenyakua ushindi kwa raundi ya kwanza.

Akiwa bado kwenye muungano na uhuru na ruto alibuni muungano wa KKK ambao ilikemewa vikali na baada ya hapo kukihama KKK na kuanza kuingilia mrengo wa jubilee kwa tuhuma za kikabila.

...Tunaona kama mdau alivosema siku moja wanasiasa kenya hueneza kampeini ambazo hazina mshiko

...lakini hivi sasa, kuna katiba npya na vyeo vipya kama gavana, seneta, mwakilishaji wa wanawake, na hizi sio nafasi za kisiasa, bali ni vyeo vya kutumikia wananchi...

..Ina maana kama taifa la kenya tuna matumaini ya kupiga hatua kimaendeleo, kwa sheria mpya ya ugatuzi...

....Siasa mbovu za familia chache nchini kushikilia nyadhifa miaka nenda rudi imefikia kikomo.
 
mkuu Kabaridi, ukweli ni kwamba kilichoshinda kenya siyo sera safi au siasa safi bali ni kabila la kikuyu na kelenjin ambao kwa muungano wao wanakuwa na a significant voting block in number and region.

Ingalikuwa sera na siasa safi hapo ingekuwa safi saaaana.

Hofu ni kwa kabila moja kuwa na hati miliki ya kutawala kenya at the same time kuwasimanga makabila mengine
 
Last edited by a moderator:

nakubali bali ukabila iko kwenye nia ya wanadamu, na hapa kenya degree zinavary katika makabila mengi na sio kulingana ni jinsi mtu binafsi amepiga hatua kiuchumi maana hata kwenye slums maskini anaeneza ukabila kwa njia fulani kulingana na siasa inayochezwa. isitoshe, mimi nafikili hata muingiliano wa wakenya kwa jumla hautamaliza ukabila bila kumaliza siasa mbaya.

haiwezekani kuhubiri kumaliza ukabila bila kuhubiri umoja wa wananchi. niseme mrengo wa cord ulikua na nia njema kumaliza ukabila lakini walikosa mbinu mwafaka au sera ya kuuzia wakenya wengi kuhofia kuwa mbinu yao ingesambaratiha taifa.

swali:

...ni nini hasa huanza ukabila katika case ya siasa za kenya?

1.ni ile dhana kuwa jamii fulani imetengwa kiuchumi na wanatumia kivuli cha ukabila kujipigia debe.
2.vilevile kikundi kingine kinatumia ukabila kujilinda kihali na mali
3.kikundi kingine kinatafuta umaarufu zaida ya vikundi vingine kwa kutumia ukabila. nk

na haya yote kwa njia moja au nyingine ni forms za ukabila ambazo ni hatari kwa taifa. dawa haswa ya kumaliza ukabila ni mfumo ambao tunao hivi sasa. uliona wale wanasiasa ambao waliitwa political comedians ama jokers walilambishwa sakafu.
 
ndugu yangu Mwita Maranya,

kuna kipengee muhimu umeshidnwa kusoma kwenye post. kama unafuatilia siasa za kenya kwa makini utaelewa namaanisha nini. kwa sasa wale ambao hawafuatilii kwa makini wanakibarua kuelewa post zangu
 
Kabaridi naye vipi?
Kwa kuwa Umeshinda umakamu wa rais ndiyo siasa za ukabila zimefika mwisho?.

Hata hivyo hongera sana, kwa hakika unaijua mizengwe ya siasa za Kenya.
 
Kabaridi naye vipi?
Kwa kuwa Umeshinda umakamu wa rais ndiyo siasa za ukabila zimefika mwisho?.

Hata hivyo hongera sana, kwa hakika unaijua mizengwe ya siasa za Kenya.

I am dreaming to become a president of kenya in the near future lakini kile tunahitaji mkuu ni serikali yenye formula ya kusema na kutenda; sasa basi.
 
Mimi sijui sana kuhusu siasa za Kenya lakini vile nimeona matokeo ya uchaguzi huu, Muheshimiwa president elect Uhuru atafanya kosa kubwa sana kisiasa na kiuongozi kama atamtupa kabisa katika duru za uongozi wa taifa aliyekuwa opponent wake mkubwa Muheshimiwa Raila! ukiangalia kwa makini Uhuru alimzidi Raila kwa si zaidi ya 10% ya kura zote hii mana yake ni nini, ni kuwa ukijumlisha kura zote idadi ya watu ambao hawana imani na Uhuru kuwa Rais wa Kenya ni 49. % na kati ya hao 46.% hawamtaki kabisa Uhuru na walichagua Raila, so ni ngumu kuongoza taifa la aina hii kama utadharau sauti ya 49.%! be a bit clever Mr President elect make a good use of Raila so you can govern Kenya to expected prosperity! hongereni ndugu zetu wa Kenya!
 
Mkuu nadhani Uhuru analijua hili na tayari ameshawakaribisha wagombea wote washirikiane kuijenga Kenya na alilisisitiza kwa kumtaja rasmi Raila, lakini kama ujuavyo ni lazima na upande wa pili nao uonyeshe uungwana kupokea mkono huo wa amani. Labda tusubiri tuone hali inavyoendelea
 
Vice president wa kenya alifanya hesabu zake vibaya kwa kuihama serikali teule ya jubilee na kuungana na cord. Sio kalonzo pekee ni wengi pia kwenye miungano mengine ambao wamelambishwa sakafu. Kwa kuungana na CORD alifikili kuwa wamenyakua ushindi kwa raundi ya kwanza.

Akiwa bado kwenye muungano na uhuru na ruto alibuni muungano wa KKK ambao ilikemewa vikali na baada ya hapo kukihama KKK na kuanza kuingilia mrengo wa jubilee kwa tuhuma za kikabila.

...Tunaona kama mdau alivosema siku moja wanasiasa kenya hueneza kampeini ambazo hazina mshiko

...lakini hivi sasa, kuna katiba npya na vyeo vipya kama gavana, seneta, mwakilishaji wa wanawake, na hizi sio nafasi za kisiasa, bali ni vyeo vya kutumikia wananchi...

..Ina maana kama taifa la kenya tuna matumaini ya kupiga hatua kimaendeleo, kwa sheria mpya ya ugatuzi...

....Siasa mbovu za familia chache nchini kushikilia nyadhifa miaka nenda rudi imefikia kikomo.

Unasemaje kuwa hivyo siyo vyeo vya kisiasa wakati wakati wau hao wanatokana na political parties, na wapigiwa kura na wananchi kila baada ya miaka mitano na wanashindana kutokana na vyama vya siasa.
 
nope, thanks

hiyo ni utani ambayo Royals amekuwa akieneza JF kwa muda sasa, i am a kenyan

lol
Kama wasomi wa JF wakifuatilia kwa umakini changizo zako humu, wallahi wewe ni Ruto. Rafiki yetu AB-Tichaz ambaye siku hizi anauguza maumivu yeye kajionesha tu kuwa yeye ni ni mshabiki wa Raila. Lakini wewe ni yule jamaa anayesemaga 'sisi hatutaki vitendaweli tunataka kupeleka Kenya mbele".
 
hebu change story line kidogo tusiangukie mtego wa panya, wewe Royals yaonekana kimpango kazuzuliwa na ruto au sio. hii si mara ya kwanza unasisitiza haya. niliunga mkono mrengo wa TNA ndio yaonekana kana kwamba usemi wangu unafanana na watu wengine kwenye muungano wa TNA. huyo jamaa unaona location yangu na yake haviendi mimi nilimo hapa mt .kenya na yeye nbi

Ab-Titchaz naye anahitaji muda kurudi hali yake ya kawaida. maana farasi yake ilikula kichapo mwisho wa uchaguzi sawa na Mekatilili lol

....poleni samaki poleni
 
Unasemaje kuwa hivyo siyo vyeo vya kisiasa wakati wakati wau hao wanatokana na political parties, na wapigiwa kura na wananchi kila baada ya miaka mitano na wanashindana kutokana na vyama vya siasa.

vyeo hivi vimetokana na ushindani kati ya miungano, lakini tofauti utagundua kama jmbo la NBI gavana alipata kidero. ukiangalia jimbo lingine kama laikipia central CORD kanyakua ushindi.

..hapo kitambo viongozi walihakikishiwa nyafidha kwa dhana ya kuwa wakuu wa kabila fulani. pia ikiwa umefuatilia pale north imenti kuna kiongozi asiye na asili ya kiafrika rahim dawood ambaye ali9chukua nafasi ya ubunge na APK.

...ndio nikaja ni hii mada kuwa wakenya wanaondoka katika fikira za kikabila na rangi kufanya uamuzi wao.

swali ni je hii sio demokrasia endelevu?!
 
ndugu yangu Mwita Maranya,

kuna kipengee muhimu umeshidnwa kusoma kwenye post. kama unafuatilia siasa za kenya kwa makini utaelewa namaanisha nini. kwa sasa wale ambao hawafuatilii kwa makini wanakibarua kuelewa post zangu

Rafiki yangu Kabaridi muzee ya kusema na kutenda nimekuelewa sana.
Nilichokuwa namaanisha ni kwamba heading inamtaja Kalonzo kuondolewa katika ulingo wa siasa lakini kwa hakika hukuweza kubainisha kwa undani ni vipi ameondolewa.
Alliance si jambo geni na kushindwa kwa CORD haiwezi kuwa sababu ya kumtoa katika ulingo wa siasa.
Naamini muda si mrefu utamuona Musyoka akiendelea kuwa juu hata kama unaamini kwamba Charity Ngilu ndiye kafanya chaguo sahihi toka huko Ukambani,usisahau kuwa ukambani wamemkataa Charity Ngilu kwenye ballot box.
 
Last edited by a moderator:
mwenzangu Mwita Maranya, kumbuka hata iwe kalonzo atabaki kuichukua taji la kuwa kigogo cha ukambani, hiyo sio faraja. kumbuka hio ndio sehemu raila amekaa miaka hizi zote na mpaka wa leo anatazama mkoloni kumpee hati miliki ya kuitawala kenya. ambayo mwisho huja na vitisho vya kidiplomasia.

ikiwa kalonzo atatarajia kuwa kiongozi wa kutegemewa ukambani, itamlazimu abadilishe mbinu au siasa zake. maana tumeshuhudia hio mbinu ya kujitwika taji la kigogo hutenganisha wananchi na serikali yao

katika serikali ya mseto unakumbuka ilibidi Raila kuchukua kejeli nyingi sana kutoka wapinzani wake alipotaka kutekeleza majukumu yake. yamanisha kalonzo atakuwa kizngiti tena kati ya serikali na jamii ya wakamba.

...kalonzo asitarajie mahakama iwapatie afueni ya kugeuza maamuzi ya urais, maana itategemea kama watakuwa na strong EVIDENCE ya uibaji kura na sio kupeleka tu tuhuma bila misingi.

isipokuwa ngilu sio mpinzani ana kila nafasi ya kujumuika katika shughuli za serikali teule utavyoona hivi karibuni
 
Back
Top Bottom