Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

Marekan watakujali pale ukiwa na faida nao tu na wakikutumia Kama spy wao siku wakiona hawakuhitaj tena wanaweza hata kukuuwa... Dr analijua hilo vizuri ndo maana hizi story znabak kusimuliwa na watu wa pemben tu ila ye yupo kama hayupo
Nakumbuka kama niliwahi kusoma humu humu jukwaani kuwa sehemu zote ulimwenguni, hawa watu huwa wanaellezwa fika kabisa kuwa UKIKAMTWA, SISI HATUKUJUI. Sasa,kama utaratibu kawaida huwa uko hivyo, kwa hili la Dr. Shika, wa-Marekani wana kosa lipi? Ni kawaida, ndiyo maadili ya kazi zao namna zilivyo
 
Jina lake halisi anaitwa lunyalula kidola makani
Na ndio jina la vyeti na elimu kwa ujumla

Walivyo washenzi ata uki-google jina lake halina info zozote.

Yaani Google wanashindwa kutambua
sasa doctor mwenye PhD ata google haikujui nani atakuamini kukupa kazi
 
Mtoa mada alikua anatililika utadhani kweli vile. Hii inshu a-z ilikua kamba.
Leo eti nayeye ni mtia nia wa kino.
 
Mkuu
Fuatilia kwa undani zaidi ili upate uhakika wa nani alimrudisha Tanzania. Kwani akitoka Moscow hadi Dar na escort. Wahusika waliofanya zoezi hili walikuwa amina nani.
 
Mtoa mada alikua anatililika utadhani kweli vile. Hii inshu a-z ilikua kamba.
Leo eti nayeye ni mtia nia wa kino.
Umenichekesha humu kuna watu wanakamba na kuna watu wanaamini, mtu anakwambia alifika kwenye jumba alilokuwa kashakiliwa ila picha ya hilo jumba anaitoa google hata kulipiga hakuweza.
RIP dr. shika uliwapa watu cha kuongelea.
 
*R.I.P DR. SHIKA😭*

Dr.Shika alikuwa ni miongoni mwa wasomi wazuri lakini bahati mbaya elimu yake haijaweza kusaidia taifa hili achilia mbali kumsaidia yeye binafsi.

Wengi walimchukulia kimzaha tangu alipoonekana kwenye tukio la mnada wa nyumba za Lugumi (mia tisa itapendeza). Makampuni ya kibiashara yalitumia umaarufu wake kama fursa ya matangazo lakini yakamuacha hohehahe asiye hata na mahali rasmi pa kuishi. Aliwahi kuripotiwa na kituo kimoja cha TV kufukuzwa kwenye nyumba aliyokua akiishi huko Tabata baada ya kushindwa kulipia kodi.

Vyombo vingi vya habari vilikuwa vikimdhihaki na vingine kumuita Kalubandika. Lakini bila shaka vilifanya hivyo pasipo kumjua kiundani *Dr.Shika.*

Ni mzaliwa wa kijiji cha Kalemela wilaya ya Busega, mkoani Simiyu. Majina yake halisi ni Louis Shika Kidola. Yeye na ndugu yake Jeremiah Shika Kidola *(marehemu pia)* walikuwa wanafunzi wenye akili sana na waliofaulu vizuri masomo yao ya sekondari kwa alama za juu na kupata ufadhili wa kusoma udaktari nchini Urusi mwaka 1984 hadi 1991 waliporejea na kuanza kutibu hospitali ya taifa Muhimbili.

Mwaka 1994 Louis Shika alirejea Urusi kujiendeleza kimasomo. Alisomea shahada ya uzamili katika magonjwa ya kuambukiza (MSc in Infectious Diseases) na udaktari bingwa wa magonjwa ya akili Master of Medicine (Psychiatry). Akiwa huko alishirikiana na wenzake kuanzisha kampuni ya usambazaji wa kemikali viwandani iitwayo Lancefort Ltd.

Kwa sasa ni moja ya makampuni makubwa ya usambazaji wa kemikali nchini Urusi, na jina la Dr.Shika lipo kwenye website yao kama Muasisi na Rais wa kwanza wa kampuni.

Inadaiwa shirika la ujasusi la Urusi (KGB) liligundua kwamba akina Shika walipata fedha za kuanzisha kampuni kutoka Marekani kama mkakati wa Marekani kudukua taarifa za Urusi. Kwahiyo baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo walikamatwa. Dr.Shika alitekwa na watu waliodhaniwa kuwa majambazi kupewa mateso makali sana ikiwemo kukatwa vidole.

Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Urusi, Patrick Chokala mwaka 2017 alinukuliwa na vyombo vya habari kwamba ilibidi kutumia mbinu za "kijasusi" kumnasua Dr.Shika na kumrudisha nchini kwa dharura. Tangu aliporejea alijiingiza kwenye ulevi wa kupindukia kutokana na msongo wa mawazo.

Kwahiyo ukifuatilia historia ya *Marehemu Dr.Shika* utagundua hakuwa "kalubandika" kama ilivyodhaniwa. Ni mtu aliyekua na maono makubwa. Kama si mipango yake kuvurugika huenda angekuwa daktari bingwa na mfanyabiashara mkubwa wa kemikali duniani.

Ni kwamba tu alijikwaa, akadondoka na hakuweza kusimama tena. Serikali ilipaswa kumsaidia kusimama lakini nayo ilimtelekeza. Kwahiyo ameishi maisha ya upweke, masononeko na msongo wa mawazo kwa muda mrefu.

Kampuni aliyoanzisha ya Lancefort Ltd ambayo kwa sasa inamilikiwa na serikali ya Urusi (ilitaifishwa) ina thamani ya $27Bil sawa na TZS 60Trilioni (Bajeti ya nchi kwa miaka miwili).
_
Kwa hiyo Dr.Shika alikuwa anajiita "Bilionea" si kwamba alikuwa anaota. He used to have money. Na hiki ndicho kilichokuwa kinamtesa maana alishindwa kukubaliana na hali yake ya sasa. Hakutaka kuamini kama aliwahi kuwa na pesa.

Kujikwaa na kuanguka ni kawaida katika maisha lakini jambo la msingi ni uwezo wa kusimama tena baada ya kuanguka. Whinston Churchil aliwahi kusema "Success is not final and failure is not fatal. It is the courage to continue that counts"
_
Mtu kama huyo hakuwa mtu wa "kumchukulia poa" hata kidogo. Serikali haikutakiwa kumtelekeza. Alipaswa kupewa nafasi nyingine. Either angerudishwa Muhimbili kutibu au angetafutiwa fursa mahali pengine ambapo taifa lingeweza kufaidi ujuzi wake na pia ingekua njia ya kumsaidia kuondokana na msongo wa mawazo na kusahau "mabilioni" yake kule Urusi.

*Pumzika kwa amani Mr. mia tisa itapendeza*

C&P from WhatsApp group.

RIP Dr. Louis Shika.

P
 
Serikali za Africa tatizo sana ubinafsi mwingi hadi inasikitisha wazungu wanatuonea huruma wanatupa mikopo bado tunawaita mabeberu do we have wrong way to go R.I.P shika
 
Serikali za Africa tatizo sana ubinafsi mwingi hadi inasikitisha wazungu wanatuonea huruma wanatupa mikopo bado tunawaita mabeberu do we have wrong way to go R.I.P shika

Hakuna Mzungu anayekuonea huruma wewe. Amka. There is Always a hidden Agenda behind: mostly economic gain. Aidha kwa haya mashirika yao ya misaada Ni ajira kwa wazungu na source of Information usw. Ndo mana huku wazungu wengi wanaochangia wanalalamika kuhusu Administration costs. Almost 80% .
 
Dr Shika nae alizingua sana kwanini aweke hela nchi za Ulaya kwanini asingeweka hata nnchini kwake Tz,Kenya au S.Africa.
 
Duuh!! Mi nikienda uko wataniua mapema sana asee siwezi acha kuwala watoto wazuri.
 
Very interesting story...
 
Serikali za Africa tatizo sana ubinafsi mwingi hadi inasikitisha wazungu wanatuonea huruma wanatupa mikopo bado tunawaita mabeberu do we have wrong way to go R.I.P shika
Mmmm mkuu never trust white guys,wao wako upande wako kimaslahi tu.Agalia Dr Shika alivyopokonywa mali zake kwa kisingizio cha ujasusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…