Baada ya kujitenga na mirathi ndugu zangu wamenitenga

Vikao vyenyewe siku hizi hata sishirikishwi na vile vya kila mwaka ambavyo tuliviweka ambapo ndugu wote tunakuwepo hata aliembali lazima aje havikaliwi cha mwaka huu naona kimepita kimyakimya
Sasa ndio unatakiwa u-initiate kikao mkutane uwaweke wazi ili waelewe na waanze kukuelewa vizuri sababu ukiendelea kukaa kimya na wao hawajui ukweli halisi inakua inakua haileti picha nzuri.

Unatakiwa kusema mbele ya hao wahusika ukweli ulivyo na wao wajibu kwamba unasema ukweli au sio ukweli, shida inaonekana ni kwamba wewe unawaogopa hao kaka zako wapigaji au unawatunzia siri na huku wao wanakuangalia na kukutangaza wewe km mbaya na haufai. Njia pekee ni kuyasema hayo kwenye kikao cha wote sio kumwambia mtu mmoja mmoja hayo yasemwe mkiwa wote mmekusanyika kwenye kikao ili muanze kuelewana na kuacha kutengana.
 
Watakapoanza kugombanaia mali waakuita. Nawe, uwatenge ili usijichafue.
 
Sawa mkuu nitaufanyia kazi ushauri wako
 
Watakapoanza kugombanaia mali waakuita. Nawe, uwatenge ili usijichafue.
Sio muda tu maana mpaka tunashiriki kuweka uongozi kaka wakubwa walitaka kuweka rehani nyumba kwa ajili ya tamaa zao dada wakashituka ndio kuanza kutushawishi sisi wengine ambao hata hatukuwa na shobo na mambo za mirathi
 
Ndugu nikimaanisha kaka na dada zangu
Nimekuelewa we hujanielewa mimi.

Waambie nduguzo mgawane, mirathi inapendeza igawiwe pale pale.. huko mbele ya safari tatizo litakuwa kubwa kwa watoto wenu na wajukuu
 
Nimekuelewa we hujanielewa mimi.

Waambie nduguzo mgawane, mirathi inapendeza igawiwe pale pale.. huko mbele ya safari tatizo litakuwa kubwa kwa watoto wenu na wajukuu
Nimeamua kukaa mbali nayo najua mishe zangu cha kushangaza bado natengwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…