Baada ya kukatika nchi nzima; umeme warejea!


Sasa unafikiri zile generator 'zetu' tutazipeleka wapi???
 
Mh! Isije kuwa ni Mungu wa Kakobe ameanza kujibu maombi yake kiawamu.
 
Huwa inauma sana Mkuu.

Hawa jamaa hawana mapenzi kabisa na nchi zaidi ya kuendeleza wizi.

Serikali lazima ielewe kuwa, Wananchi sasa wanafahamu kuwa CCM ni chama kilicho kosa dira, mwelekeo, na upendo kwa wananchi wake. Na mwaka huu lazima atolewe mtu nishai, wapende au wasipende.

Habari za kukosa maji mtera ni upuuzi mtupu usio na mwelekeo. Habari za Richmond ni utumbo mtupu usio na thamani.

Dunia ya leo, si tegemezi kama ile dunia ya ujima. Tungependa hawa CCM watueleze, ni kwanini umeme unakatika wakati nchi ina upepo?
 
Sasa unafikiri zile generator 'zetu' tutazipeleka wapi???
Pamoja na kuwa na mito yote inayotuzunguka na rasilimali nyingi tulizonazo bado hata hatuwezi tukaumiza vichwa japo kidogo tu tuone tutajikwamua vipi na tatizo la nishati.Inabidi tufike mahala tukalitendea taifa letu haki ambapo ni pamoja na kuondoa kero kama hizi na hata tukafikiria kuwa mzee mwanakijiji kule aliko na wazee wenzake waache kukata magogo kwa ajili ya mkaa kwa kuwasambazia umeme vijiji.
 
Mimi niko Mbeya umeme ulikatikatika saa 1:00 jioni mkoa mzima wa Mbeya, nikajua sasa hapa ngoja tusubiri isije ikawa kama alivyosema Askofu KKB kuwa ataombea umeme usiwake,

Kama umeme umekatika Mbeya maana yake hata Iringa itakuwa hivyo.
 
Sasa unafikiri zile generator 'zetu' tutazipeleka wapi???

Naam watashuka tena ili kupigia tena debe ununuzi wa mitambo ya Richmonf ambayo iliingia nchini kifisadi. "Serikali imesema tena kuna umuhimu mkubwa wa kununua mitambo ya Richmond ili kupambana na hali mbaya ya umeme inayoikabili nchi. Serikali imesema mitambi hiyo ikinunuliwa basi itapunguza kwa kiasi kikubwa sana tatizo kubwa la umeme lililopo nchini." Halafu kwenye kauli kama hizi hukuti jina la mtu hata siku moja kama ni Kikwete au Ngeleja ambaye ametoa kauli hii siku zote itakuwa ni kauli ya lile jinamizi linaloitwa SERIKALI.
 
Mimi niko Mbeya umeme ulikatikatika saa 1:00 jioni mkoa mzima wa Mbeya, nikajua sasa hapa ngoja tusubiri isije ikawa kama alivyosema Askofu KKB kuwa ataombea umeme usiwake,

Kama umeme umekatika Mbeya maana yake hata Iringa itakuwa hivyo.


Mbona nilisikia alishakubali Tanesco wapitishe nyaya karibu na kanisa lake..au alibadili mawazo?

 

Mbona nilisikia alishakubali Tanesco wapitishe nyaya karibu na kanisa lake..au alibadili mawazo?


Hakukubali.... ila imebidi asalimu amri..... nguvu ya dola...na nasikia akasema atapitisha maombi ili usiwake...
 
Heri yangu mimi basi, kwa mtaji huu. Hata nikirudi Bongo I will still be "running on solar cells"!

Kweli haiingii kichwani.
 
mikoa mbalimbali imeanza kuripoti kurudi kwa umeme.. nadhani hali itakuwa imetengemaa
 
Tungependa hawa CCM watueleze said:

Wewe sasa umechanganyikiwa, yaani waache kujiandaa na uchaguzi waje kukueleza habari za kukatika kwa umeme are you serious! Hivi watanzania mmelogwa?? Kwanza watakwambia watanzania wangapi wanaotumia umeme, sio zaidi ya asilimia kumi, katika hawa wanaopiga kura hawazidi asilimia 18% ya wapiga kura, so wa nini nyie? Imekula kwenu hadi limbwata la CCM litakapo-expire!!
 

uwe unaongea mambo ya maana na wewe .sio unakuwa na chuki za kipumbavu na watu.Umeme ukatike unamhusisha Lowassa na Rostam...umaskini wa mawazo kitu kibaya sana
 

Tatizo sio serikali haijui ifanye nini..ukiwapa siemens tender wataishia kufanya kazi coz ni kampuni inayojali reputation yake pia na huwa wanatoa hongo ndogo sana kwa viongozi na chama au no hongo kabisaaaa...kwaiyo inakuwa poa kuunda kampuni feki 100% owned by pesa za walipa kodi na kuilipa. Angalia TRL kwani serikali imeshindwa kuongea na national rail etc etc za uingereza au marekani..lakini waliona bora kuwapa wahndi ambao wakawabail out kwa hela ya walipa kodi...Tanzania umaskini wakujitakia!!
 
uwe unaongea mambo ya maana na wewe .sio unakuwa na chuki za kipumbavu na watu.Umeme ukatike unamhusisha Lowassa na Rostam...umaskini wa mawazo kitu kibaya sana

Unajifanya hujui ni nani katika nji hii anaegombania kwa udi na uvumba kuwa dalali kati ya tanesiko na walaji wa umeme? Ni hawa hawa kina RA na EL!!!
 

Swali la nyongeza mheshimiwa Ngeleja wakati akiperuzi hii thread, ni kwa nini hakuna backup generators au power station kuserve wakati wa emergencies kama hizi?
 
Lakini hivi kwa nini tuna gridi ya taifa? Kwa nini kila mkoa usiwe na chanzo chao cha umeme? Mimi sijui sana haya mambo ya umeme labda mnaojua mtanielewesha....maana kila kukiwa na tatizo kwenye hiyo gridi ya taifa basi sehemu kibao kunakuwa hakuna umeme...WTF?
 
Mambo ya Kakobe hayo yameanzaa alisema maajabu yatatokea, ndio hayo sasa. Alikuwa anazumzingia ule umeme wa pale Tanangozi leo Mchana
 
MM Naomba Number ya Ngeleja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…